ANGALIA LIVE NEWS

Tuesday, April 21, 2015

BALOZI WA MALAWI NCHINI TANZANIA AMTEMBELEA WAZIRI WA UCHUKUZI OFISINI KWAKE LEO MCHANA

Waziri wa Uchukuzi, Samuel Sitta akimsikiliza Balozi wa Malawi nchini Tanzania, Hawa Ndilowe alipomtembelea Waziri huyo ofisini kwake. Waziri wa Uchukuzi na Balozi huyo wamejadili masuala mbalimbali yanayohusu sekta ya Uchukuzi na Balozi huyo aliipongeza Wizara kwa kutekeleza vyema miradi inayotekelezwa chini ya Mpango wa Matokeo Makubwa sasa(BRN).
Waziri wa Uchukuzi, Samuel Sitta akisisita jambo kwa Balozi wa Malawi, Hawa Ndilowe, alipomtembelea ofisini kwake leo mchana kujadili masuala mbalimbali yanayohusu sekta ya Uchukuzi. Wa pili kutoka kulia ni Afisa Usafirishaji Mwandamizi,kutoka Wizara ya Uchukuzi, Bw. Biseko Chiganga.
Waziri wa Uchukuzi, Samuel Sitta, akimuonyesha mafanikio ya sekta ya Uchukuzi, Balozi wa Malawi, Hawa Ndilowe, alipomtembelea ofisini kwake leo mchana. (Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini-Uchukuzi)

No comments: