ANGALIA LIVE NEWS

Sunday, April 19, 2015

DIAMOND PLATNUMZ: MBUNGE HALIMA MDEE NI MZIGO JIMBO LA KAWE


Msanii maarufu nchini mwenye mafanikio makubwa katika sanaa ya mziki wa kizazi kipya, Diamond Platnumz, amevunja ukimya wake juu ya ubovu wa barabara iendayo Madale ambayo ipo kwenye jimbo la Kawe chini ya Halima Mdee.
Msanii huyo ameelekeza lawama zake kwa mbunge huyo wa kupitia tiketi ya CHADEMA kwa kuwa Halima Mdee aliahidi wananchi wa jimbo hilo kuwa katika kipindi chake cha ubunge atahakikisha barabara hiyo inajengwa kwa kiwango cha lami, lakini hadi hii leo barabara imejaa tope tu!

Diamond alieleza masikitiko yake huyo kupitia katika kituo cha Clouds TV pale alipoulizwa swali kuhusu makazi yake mapya yaliyopo katika jimbo la Kawe na ndipo hapo akafunguka kuhusu suala hilo la kero ya barabara ambalo lina muda mrefu alijashughulikiwa na mbunge Halima Mdee.

3 comments:

Anonymous said...

Diamond, toa mchango ili road itengenezwe. Wabunge kazi yao siyo ku-construct roads!!!

Anonymous said...

Kazi ya wana wa nchi ni kutoa maoni juu ya utendaji wa wabunge pamoja na viongozi wa kitaifa. Si kazi ya wana wa nchi kutoa michango kwa maendeleo ya nchi. Kodi tunalipa zinakwenda wapi?

Mdau hapo juu funguka - hutakiwi kutoa michango kujenga balabala, hospitali, kuzoa taka mitaani - mbuge anatakiwa afanye kazi na watendaji kuanzia ngazi ya taifa, mkoa na wilaya kuleta maendeleo kwa watu wealiompigia kula.

Kama Mdee hafanyi kazi basi hatumtaki kawe au kokote tanzania.

Anonymous said...

Muulizeni Diamond analipa kodi ya mapato (income tax ) kiasi gani?,je,anatambua kuwa shughuli za maendeleo zinachangiwa na kodi?