Waziri wa Uchukuzi,Samwel Sitta akionyesha baadhi ya Ripoti za uchunguzi za mamlaka ya Bandari,TPA na Ripoti ya shirika la Reli jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Uchukuzi,Samwel Sitta akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana kuwasimamisha baadhi ya watendaji wakuu wa kampuni ya Reli hapa nchini uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Wizara hiyo jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya Waandishi wa Habari walio hudhuria katika mkutano wa Waziri wa Uchukuzi,Samwel Sitta katika wizara hiyo jijini Dar es Salaam.Picha na Avila kakingo
Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii
Akitangaza maamuzi hayo ya kusimimishwa kwa Mkurugenzi huyo ljijini Dar es Salaam baada ya ripoti ya kamati iliyoundwa na Waziri wa Uchukuzi (ambaye sasa ni Waziri wa Afrika Mashariki), Dk. Harrison Mwakyembe, Waziri wa Uchukuzi,Samwel Sitta amesema ameshtushwa na malipo hayo kwani yamekiuka manunuzi ya umma kwani mkataba wake ulikuwa TRL ilipe nusu ya asilimia 50 lakini matokeo yake mabehewa yamelipwa yote.
Amesema mabehewa 120 yaliyofika nchini yakiwa yana kasoro aliyazuia baada ya kubaini hivyo lakini TRL ilikuwa imeshalipa fedha yote katika mazingira hayo yanaonyesha mkataba una dalili ya hujuma.
Waliosimamishwa wengine ni Mhandisi Mkuu wa Mitambo TRL,Ngosomwile Ngosomiles,Mhasibu Mkuu,Mbaraka Mchopa ,Mkaguzi Mkuu wa Ndani Jasper Kisiraga pamoja na Meneja Mkuu Ferdinand Soka.
Kamati ya uchunguzi kwa watendaji hao kwa kuidhinishwa kwa kulipwa kwa mabilioni ya Shilingi itaongozwa na Ofisi ya Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG),Taasisi ya Kupambana na Rushwa (Takukuru),Mamlaka ya udhibiti wa Ununuzi katika sekta ya Umma (PPRA),pamoja na Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali.
No comments:
Post a Comment