KIJANA MWENYE UMRI WA MIAKA 20 ALIYETAMBULIKA KWA JINA LA FADHIL SIKAPUNDWA, MKAZI WA NAMTAMBALALA WILAYANI MOMBA ALIUAWA PORINI KWA KUPIGWA FIMBO SEHEMU MBALIMBALI ZA MWILI WAKE NA WATUHUMIWA WALIOTAMBULIKA KWA MAJINA YA 1. SHADRACK SIMBEYE (16) 2. JOB JOHN (21) NA 3. MASUOD SIMWAKA (18) WOTE WAKAZI WA NAMTAMBALALA WILAYANI MOMBA.
TUKIO HILO LIMETOKEA MNAMO TAREHE
19.04.2015 MAJIRA YA SAA 19:00 JIONI HUKO KATIKA KIJIJI CHA
NAMTAMBALALA, KATA YA NZOKA, TARAFA YA NDALAMBO, WILAYA YA MOMBA, MKOA
WA MBEYA. INADAIWA KUWA, CHANZO CHA TUKIO HILO NI TUHUMA ZA WIZI WA
VIATU, SIMU NA NGUO. WATUHUMIWA WAMEKAMATWA NA UCHUNGUZI ZAIDI WA TUKIO
HILI UNAENDELEA.
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA
KAMISHNA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA
JAMII KUACHA TABIA YA KUJICHUKULIA SHERIA MKONONI KWANI KUFANYA HIVYO NI
KINYUME CHA SHERIA NA BADALA YAKE WAJENGE TABIA YA KUWAFIKISHA KATIKA
MAMLAKA HUSIKA WATUHUMIWA WANAOKAMATA KWA TUHUMA MBALIMBALI KWA HATUA
ZAIDI ZA KISHERIA.
KATIKA TUKIO LA PILI:
MWANAMKE MMOJA MKAZI WA KIJIJI CHA
IYENGA ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA PILLY MGALA ALIMUUA MUME WAKE AITWAYE
AMADI MWASHAMBWA, (42) MKAZI WA KIJIJI CHA IYENGA KWA KUMCHOMWA KISU
KIFUANI.
AWALI MNAMO TAREHE 19.04.2015
MAJIRA YA SAA 21:00 USIKU HUKO KATIKA KIJIJI CHA IYENGA, KATA YA ISANSA,
TARAFA YA IGAMBA, WILAYA YA MBOZI MWANAMKE HUYO ALIMJERUHI MUME WAKE
KWA KUMCHOMA KISU KIFUANI NA KUPELEKEA KUKIMBIZWA KATIKA ZAHANATI YA
KIJIJI CHA IYENGA KWA MATIBABU. KUTOKANA NA MAJERAHA ALIYOYAPATA MNAMO
TAREHE 20.04.2015 MAJIRA YA SAA 13:00 MCHANA ALIFARIKI DUNIA WAKATI
ANAPATIWA MATIBABU.
CHANZO CHA TUKIO HILO NI UGOMVI
ULIOTOKANA NA WIVU WA KIMAPENZI BAADA YA MAREHEMU KUMTUHUMU MKE WAKE
KUWA SIO MWAMINIFU KATIKA NDOA YAO. MTUHUMIWA ALIKIMBIA MARA BAADA YA
TUKIO NA MSAKO MKALI UNAENDELEA WA KUMTAFUTA.
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA
KAMISHNA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA
WANANDOA KUTATUA MIGOGORO YAO KWA KUKAA MEZA MOJA NA KUFIKIA SULUHISHO
ILI KUEPUKA VITENDO VYA KUJICHUKULIA SHERIA VINAVYOWEZA KUSABABISHA
MADHARA NA MATUKIO KAMA HAYA YA MAUAJI.
TAARIFA ZA MISAKO:
JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA
LINAMSHIKILIA KIJANA MMOJA MKAZI WA FOREST YA ZAMANI ALIYEFAHAMIKA KWA
JINA LA EMANUEL SAMWEL (28) AKIWA NA NOTI BANDIA AMBAZO KAMA ZINGEKUWA
HALALI ZINGEKUWA NA THAMANI YA TSHS 325,000/=.
MTUHUMIWA ALIKAMATWA MNAMO TAREHE
20.04.2015 MAJIRA YA SAA 16:00 JIONI HUKO ENEO LA ISYESYE, KATA YA
ISYESYE, TARAFA YA IYUNGA, JIJI NA MKOA MBEYA AKIWA KWENYE HARAKATI ZA
KUJARIBU KUWEKA PESA HIZO KWENYE AKAUNTI YAKE YA TIGO-PESA KWENYE DUKA
LA MARY PATRICK (32) MFANYABIASHARA NA MKAZI WA ISYESYE.
NOTI HIZO ZILIKUWA NA NAMBA DT.
2937833 NOTI 6, BV 2937839 NOTI 10, DT 4243042 NOTI 4, BF 1547948 NOTI
5, BV 4243044 NOTI 8, AA 4243045 NOTI 18, DT 1547949 NOTI 5 NA BC
2937831 NOTI 10. TARATIBU ZA KUMFIKISHA MAHAKAMANI ZINAENDELEA.
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA
KAMISHNA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA
JAMII KUENDELEA KUTOA TAARIFA KATIKA MAMLAKA HUSIKA PINDI WAONAPO
VIASHIRIA VYA UHALIFU AU WANAPOMTUHUMU MTU/WATU ILI HATUA STAHIKI
ZICHUKULIWE DHIDI YAO.
Imesainiwa na:
[AHMED Z. MSANGI – SACP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA
No comments:
Post a Comment