Jumuiya ya Watanzania wa New York, New Jersey, Connecticut na Pennsylvania ikishirikiana na Ubalozi wa Tanzania Umoja wa Mataifa kwa pamoja na udhamini wa Miss Tanzania USA. Tunapenda kuwataarifu wanajumuiya wote kuwa kutakuwa na BBQ maalum kwa ajili ya kusherehekea Sikukuu ya Muungano wetu/Tanzania Day ambayo ilikuwa April 26,1964. Shime tujitokeze kwa wingi kusherehekea siku yetu hii adhimu itakayofanyika siku ya Jumamosi tarehe 2 Mei 2015 kuanzia saa Saba mchana Roosevelt Island. Kama kawaida yetu tunaomba wanajumuiya kuchangia ili kufanikisha event yetu kwa kuleta vinywaji, chakula ama mchango kiasi utakachojaaliwa. Bingwa wa BBQ Chef Lucas atakuwepo. Karibuni tuungane na Mabalozi wetu kusherehekea Muungano wetu wa kihistoria.
Kwa maelezo zaidi unaweza kuwasiliana kupitia number hizi hapa chini.
Katibu/Mariam Abuu#+(1914)-316-2814
Mwkt/Hajji #+(1347)-623-8965
Bahia#+1(347)663-0781
Gaston#+1(646)-359-2367
Uongozi.
Kamati ya Uongozi wa Jumuiya ya Watanzania NY
Address ni hii:
The Octagon, 888 Main Street, NY 10044
12 comments:
Wengine tunaogopa kuja maana last year Lucas alichoma kuku na alimwagia au kawapaka maji yenye rangi kama ya bia/beer na la kushangaa hakukatazwa na viongozi hili rimetuuzi sana na pia walikuja wakina mama na kaka Wageni wa kiislam na waliondoka na jambo akilini
That was seasoning not a beer
We bonge la fala kweli. Kuna mtu alikufumbua hilo domo na kukuwekea hao kuku au ni wewe kuwamezea mate and then unajilaumu baada ya kushibisha tambi lango. Berbeque kama kawa just bring your appetite and appetizer kwa sana tu.
Si busara kumtukana alietoa maoni ni vyema kujirekebisha kama kweli kimetokea kitendo hicho maana umoja ni watu na wakianza kuona kasoro kama hizi ni athari kwa jumuiya yetu ya Tanzania
Ni kweli ila hakuwa Lucas, aliondoka kidogo but yule aliemshikia ndio alifanya iyo kitu. Ila kwenye sherehe kama hii tuwe makini ili kila mtu awe powa.
wabongo was USA you have so much time to celebrate this and that. You all think you are still in Bongo? Come back then.
We Hajji, si ninasikia uenyekiti wako unaisha tarehe 30 April? Saa hiyo tarehe 2 Mei, wewe ni kama nani?
Duh halafu mnasema dmv wana majungu. Kwani tatizo ni nini? Si mkale nyama tu hautaki susa
Wanchama wote wa NYTC- someni katiba ya New York Tanzania Community neno kwa nemo na msitari kwa msitari. Hiyo April 30 imetoka wapi na hiyo tarehere 2 Mei ina uhusiano gani na Hajji isiopkuwa huyu anninmouss wa april 29, 2015 at 11.17 anataka vurugu tu. Wanachama wote wanajua kwamba viongozi wa jumuia watamailza kipndi chao baada ya uchaguzi wa waendashaji wa Bodi wapya amambao watakuwa wamechaguliwa na wanajumuia.
Tunakuja kula nyama tukijua nyinyi si viongozi tena. Uchaguzi lini?
Uchaguzi unaweza kufanyika siku yeyote ile wanachama watakapo amua. Chagueni siku nzuri tu na nyama nyingi zitachomwa.
Wee nawe umeishiwa hoja! Ratiba ya uchaguzi mpaka wanachama waamue? Katiba haielekezi?
Post a Comment