Majeruhi wa ajali hiyo wakiokolewa.
Wanachama Saba (7) wa Klabu ya Simba ya Dar es salaam kutoka tawi la Mpira na Maendeleo (maarufu kama Simba UKAWA) ambalo limewahi kutangazwa kufutwa wamefariki dunia katika ajali ya basi jana Aprili 3, mkoani Morogoro.
Akizungumza mmoja kati ya mashabiki hao Frank Ngowi amesema ajali hiyo iliyotokea eneo la Mkundi nje kidogo ya manispaa ya Morogoro imetokana na gari lao kupishana na gari lingine na kesha kupoteza muelekeo.
Ajali hiyo imetokea wakati wanachama hao wakiwa katika basi lao kuelekea Shinyanga kwa ajili ya kuipa nguvu Klabu yao ya Simba ambayo inatarajiwa kushuka katika dimba la CCM Kambarage kuikabili Kagera Sugar katika mchezo wa ligi Kuu Tanzania Bara kesho..
Vifo hivyo vimefikia 7 baada ya watano kufa palepale na wengine wawili waliokuwa majeruhi kufariki katika hospitali ya mkoa wa Mororgoro walipokuwa wakipewa matibabu.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro SACP Leonard Paul amethibitisha habari hizi na kusema kuwa majeruhi wamebaki 13 na kufanya vifo kufikia saba hadi majira ya saa 2 usiku wa April 03.
NA EATV REDIO
No comments:
Post a Comment