Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Morogoro, Leonard Paulo, akiwaonesha waandishi wa habari ( hawaonekani pichani) milipuko hatari aina ya ' Water explosives gel ' iliyokamatwa jana usiku kutoka kwa watuhumiwa tisa waliokuwa wamehifadhiwa ndani ya msikiti wa Suni uliopo Tarafa ya Kidatu, wilayani Kilombero mkoani Morogoro.
Watu 10 wanashikiliwa na polisi mkoani Morogoro baada ya kukamatwa msikitini wakiwa na milipuko 30, sare za jeshi na bendera nyeusi inayodaiwa kutumiwa na kundi la wapiganaji wa Al Shabaab wa nchini Somalia.
Akizungumza na waandishi wa habari, Kamanda wa polisi mkoani Morogoro, Leonald Paul alisema tukio hilo limetokea juzi (Aprili 14 mwaka huu) majira ya saa 3.30 usiku katika kitongoji cha Nyandero, tarafa ya Kidatu wilayani Kilombero. Aidha alisema siku ya tukio polisi walipata taarifa kutoka kwa raia wema kuhusu watu hao na kwamba walitaarifiwa kuwa wanajihusisha na matukio mbalimbali ya uhalifu na polisi waliamua kufatilia nyendo zao.
Kamanda huyo alisema walianza kuwasaka watu ambao walipata taarifa wapo katika Msikiti wa Suni uliopo Kidatu.“Polisi walipofika katika msikiti huo waliuomba uongozi wa msikiti huo kuwatoa watu wote waliokuwa msikitini ili kuweza kubaini watu ambao wanatiliwa mashaka,”
1 comment:
WANAOTOA TAARIFA WAPEWE ZAWADI KWANI ALSHABAB NI WATU WALLAANIWA.KITABU GANI KIMEANDIKA UWE UENDE PEPONI ? MNATUTIA AIBU WAISLAM WENZENU
Post a Comment