Madaktari wanaswa wakisinzia kazini huku wagonjwa wakisubiri matibabu
Je umewahi kushudia daktari akisinzia Hospitalini huku wagonjwa wakimsubiri ?
Katika mataifa mengi ya Afrika na Marekani Kusini ,kuna uhaba mkubwa wa madaktari jambo linalowalazimu madaktari na wauguzi wachache walioko kufanya kazi ya ziada ilikuwatuza wagonjwa.
Si ajabu kumsikia daktari anayehudumu katika hospitali ya umma ndiye yuleyule anayekimbia kumhudumia mgonjwa katika hospital ya kibinafsi iliapate pesa za ziada.
Je ni Uroho ama Uhaba wa madakari ?
Je mtizamo wako ni upi kinawapelekea madaktari hao kufanya kazi hata zaidi ya saa 8 zinazopendekezwa ?Je ni Uroho ama Uhaba wa madakari ?
Si Aghalabu visa vya madaktari kufanya makosa wakiwa katika vyumba vya upasuaji na hata mara nyengine katika vyumba vya wagonjwa mahututi kwa sababu ya uchovu.
Huko Mexico wagonjwa na jamaa zao wameanzisha kampeini ya kuwatetea wanafunzi wanaojifunza kazi.
Waliwapiga picha madaktari wakisinzia na kuzichapisha katika mitandao ya kijamii.
''inakuaje daktari ambaye anawajibu wa kuwatunza wagonjwa 12 anasinzia kazini''
''Hii ni kama rubani kusinzia ndege ikiwa angani ''anasema mwandishi wa blogu aliyechapisha picha hizo.Hii ni kama rubani kusinzia ndege ikiwa angani ''anasema mwandishi wa blogu
Watu waliochangia mjadala huo walidai kuwa madaktari wakuu wamekwenda kulala na kuwaachia wanafunzi wao kazi chungu nzima.
Baada ya mjadala huo katika vyombo vya habari ilibainika kuwa madaktari hao hufanya kazi wakati mwengine hata zaidi ya saa 36 bila mapumziko.
Wengi waliwashtumu madaktari waliohitimu wakisema kuwa wanawatelekeza wagonjwa wao kufuatia kuimarika maradufu kwa mishahara yao.
Je haya yamewahi kukupata?
Source: BBCSwahili
No comments:
Post a Comment