ANGALIA LIVE NEWS

Sunday, May 17, 2015

TRENI YA DELUXE KWENDA KIGOMA YAAHIRISHWA HADI KESHO JUMATATU SAA MBILI USIKU

Uongozi  wa Kampuni ya Reli  Tanzania  (TRL ) unasikitika kuwataarifu abiria  wa treni ya Deluxe ya kwenda  Kigoma leo Mei 17, 2015 saa 2 usiku kuwa safari hiyo imeahirishwa  hadi kesho Jumatatu Mei 18, 2015 saa 2 usiku. 

Kwa mujibu wa taarifa hiyo sababu za kuahirishwa  zinatokana na ajali mbili mfululizo za treni za mizigo.

Ajali ya kwanza ilitokea asubuhi saa 1:30 maeneo ya Stesheni ya Ngeta mkoa wa Pwani na ya pili saa 5 asubuhi maeneo ya Stesheni  za Kinguruwila  na Morogoro!

Ajali hizo zimehusisha kuanguka kwa mabehewa manne ( Ngeta ) na kuacha njia behewa moja (Kinguruwila )! Treni zote mbili zilikuwa zikielekea    bara!

Tayari  wahandisi na  mafundi  wa TRL  wako katika maeneo  ya tukio kwa ajili ya kazi ya kuyaondosha mabehewa yaliopata ajali na pia kukarabati njia ili ifunguliwe haraka na kurejesha mawasiliano ya njia ya reli katika hali ya kawaida. 

Kutokana na uzito wa kazi hiyo ya ukarabati njia ndio sababu kuu iliyopelekea safari ya Deluxe iahirishwe hadi kesho usiku!  

Wakati huo huo taarifa imeongeza kusema kuwa ajali hiyo imeathiri  urejeshaji wa vichwa viwili vya treni ya Jiji ambavyo havotoweza   kufika Dar kwa wakati na hivyo kesho huduma ya treni ya Jiji haitokuwepo. 
Vichwa hivyo vya treni vilikuwa katika ukarabati wa kawaida katika karakana kuu ya TRL  Morogoro!  Atakayesoma  taarifa hii amuarifu nwenzake!  

Uongozi wa TRL unasikitika kwa usumbufu utakaojitokeza!

Imetolewa na Afisi  ya Uhusiano kwa niaba ya Kaimu Mkurugenzi  Mtendaji
Mhandisi Elias Mshana
Dar es Salaam, 
Mei 17, 2015

No comments: