Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki kujaza maji kwenye madumu mara baada ya kutembelea mradi wa kusambaza maji Magu mjini,Pichani kushoto ni Mkuu wa mkoa wa Mwanza Mhe. Magessa Mulongo.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na Vijana wa Boda Boda Magu mjini wakati wa uzinduzi wa shina la Wajasiriamali la waendesha Boda Boda wa UVCCM Magu Mjini,Katibu Mkuu wa CCM aliwapongeza vijana hao kwa uamuzi wa kuanzisha umoja wao na kuwataka kufanya kazi kwa bidii ,Umoja huo una vijana 80 na wote ni madereva wa Boda boda.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akipandisha Bendera ya Chama Cha Mapinduzi mara baada ya kuzindua shina la Vijana wajasiriamali la waendesha pikipiki Magu mjini.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza wakati wa kikao cha Halmashauri Kuu ya CCM Wilaya ya Magu.
Katika Kikao hicho Katibu Mkuu wa CCM amewajia juu Viongozi wanaotumia vibaya nafasi zao kwa kujifanya maarufu zaidi ya Chama alisema "Hakuna mtu maarufu zaidi ya CCM huku akisema kuna watu wanaona kama wamekiteka hiki chama nyara na kukiweka kwenye kikapu na kuzunguka nacho, Hatutokubali hilo litokee" aliendelea kusema bora mtu aende upinzani kulikoni kuwa na sisi halafu anatuumiza.
Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Magu Ndugu Isaac Zabron akizungumza wakati wa Kikao cha Halmashauri Kuu ya CCM wilaya ya Magu.
Kikundi cha Magu One Theatre kikitumbuiza kwenye uwanja wa Sabasaba kabla ya Katibu Mkuu wa CCM hajahutubia.
Kikundi cha ngoma za asili kikionyesha umahiri wa kucheza ngoma kwenye viwanja vya saba saba.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akipitia taarifa muhimu kabla ya kuhutubia kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika viwanja vya saba saba Magu mjini.
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mwanza Mhe. Antony Diallo akisalimia wananchi waliojitokeza kwa wingi kwenye uwanja wa mkutano Saba saba kabla ya kumkaribisha Katibu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana kuhutubia wananchi wa Magu mjini.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wananchi kwenye viwanja vya saba saba Magu mjini.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akimpokngeza kijana Zakaria Andrew (katikati) kwa uamuzi wake wa kumjengea nyumba mama yake mzazi (kushoto) kwa kutumia kikundi cha vijana wajasiriamali wapatao 40 wanaofyatua matofali katika kijiji cha Ilungu kata ya Nyegogo wilayani Magu.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki kufyatua matofali katika kijiji cha Ilungu kata ya Nyegogo wilayani Magu.
Katibu Mkuu wa CCM akibeba tofali mara baada ya kufyatua.
Katibu Mkuu wa CCM akiangalia nyumba iliyotengenezwa kwa matofali ya bei nafuu.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na Mwenyekiti wa Tawi la Lugeye Ndugu Yegela Mwedeya mara baada ya kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa ofisi ya Tawi.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akipata maelezo kutoka kwa Mhandisi wa maji wa Wilaya ,Injinia Rutta Merchades alipotembelea chanzo cha maji Nyanguge wilayani Magu.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiangalia pampu ya kusukumia maji kutoka kwenye chanzo cha maji ya ziwa Victoria,kushoto ni Mhandisi wa maji wilaya Injinia Rutta Merchades akitoa maelezo namna mradi huo utavyofaidisha vijiji vitatu.
Wakazi wa Nyanguge wakisubiri maji kuzinduliwa na katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana ambaye yupo kwenye ziara ya mkoa wa Mwanza ya kukagua ,kuhimiza na kusukuma utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya CCM.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiweka jiwe la msingi la uzinduzi wa mradi wa Maji Nyanguge.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akimtwisha ndoo ya maji kama ishara ya kuzinduliwa kwa huduma za maji Bi.Yustina mkazi wa Nyanguge.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisalimiana na Afisa Tabibu wa Kituo cha Afya Kisesa Dk. Charles Nyaga wakati wa kutembelea na kuona maendeleo ya ujenzi wa jengo la X-ray.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akimsalim fundi Raina Lucas anayeshiriki ujenzi wa jengo la x-ray katika kituo cha afya Kisesa.
Tangazo linaloonyesha huduma kwa wazee bure katika kituo cha Afya Kisesa wilayani Magu.
Kikundi cha Ngoma ya asili kikionyesha umahiri wa kucheza na Chatu kwenye uwanja wa mikutano Kisesa kabla ya katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana kuhutubia
Mkuu wa Mkoa wa Mwana Mhe. Magessa Mulongo akihutubia wakazi wa Kisesa .
Wakazi wa Kisesa wilayani Magu wakimsikiliza Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana alipokuwa akihutubia kwenye mkutano wa hadhara ambapo aliwaambia wananchi hao kuwa makini wanapoingia amkubaliano yeyote hasa yanayohusiana na masuala ya ardhi na halmashauri kwani kumekuwa na matatizo makubwa katika upatikanaji wa viwanja wakati vilishalipiwa na watu.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisisitiza jambo wakati wa mkutano wa hadhara Kisesa.
Katibu Mkuu wa CCM akipokea kadi kutoka kwa aliyekuwa Mwenyekiti wa BAWACHA Bi. juliana Kachidu aliyeamua kurudi CCM kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye viwanja vya Kisesa ambapo zaidi ya wananchama 53 kutoka vyama vya upinzani walijiunga na CCM wakiwemo Chadema 28 na ACT 12 na wengine kutoka vyama vingine.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinan akipokea kadi zinazorudishwa na wanachama walioamua kutoka upinzani na kujiunga na CCM.
Wakazi wa Kisesa wakifuatilia mkutano.
Katibu Mkuu wa CCM akionesha kadi zilizorudishwa kutoka upinzani
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akimkabidhi kadi ya CCM aliyekuwa Mwenyekiti wa Baraza la Wanawake la Chadema Wilaya ya Magu Bi. Juliana John Kachidu kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika Kisesa wilaya Magu mkoani Mwanza.
(Picha na Adam Mzee)
1 comment:
Sawa mh. Ila mwenzio NAPE ameuambia umma wa WaTanzania kuwa tunahakilisha tunashinda hata kwa goli la mkono!! Ninwazi kabisa mnimunza kutaka kuiba kura ziko wazi sana je kweli mnaitakia mema Tanzania?? Tusidanganyane kwaninhata daftari linaonekana kufanyiwa hujuma za kila namna kuandikisha mamluki!! Msiipeleke Tanzania pabaya.
Post a Comment