Sherehe hizo zimepangwa kufafanyika Juni 16 kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee, jijini Dar es Salaam na zitaenda sambamba na utoaji wa tuzo kwa wachezaji bora na uzinduzi wa kitabu cha Historia ya Yanga kilichoandikwa na Peter Ching’ole.
MAMBO ya fedha bwana! Klabu ya Yanga inatarajiwa kutumia kiasi cha Sh96 milioni kwa ajili ya sherehe zake za ubingwa wa Ligi Kuu Bara ilioutwaa hivi karibuni.
Sherehe hizo zimepangwa kufafanyika Juni 16 kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee, jijini Dar es Salaam na zitaenda sambamba na utoaji wa tuzo kwa wachezaji bora na uzinduzi wa kitabu cha Historia ya Yanga kilichoandikwa na Peter Ching’ole.
Mwenyekiti Kamati ya maandalizi ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Yanga Tawi la Tabata Kisiwani, Brito Burure, aliliambia Mwanaspoti akisema: “Mipango yote kwa ajili ya kufanisha shughuli hiyo, imefikia pazuri.
“Lengo ni kuwakutanisha Wanayanga nchi nzima na kusheherekea mafanikio ya klabu yao kwa pamoja.
“Lakini tunataka kuwapongeza wachezaji wetu kwa kuwapa tuzo kwa kazi nzuri waliyofanya hadi kuwa mabingwa na watatakiwa kufika kufurahia ushindi huo pamoja na familia za.”
Miongoni mwa wachezaji wanaotarajiwa kutunukiwa tuzo hizo ni Mfungaji Bora wa Ligi Kuu, Simon Msuva, pamoja na viongozi na makocha waliofanikisha Yanga kutisha katika msimu huo ulioisha.
Kuhusu kitabu hicho alisema kimebeba simulizi ya historia nzima ya klabu hiyo.
Kwa upande wa mwandishi wa kitabu hicho cha Yanga, Ching’ole alisema: “Nimeamua kuandika kitabu hicho, ili Wanayanga waitambue klabu yao kwa undani zaidi.”
CREDIT:MWANASPOTI
No comments:
Post a Comment