ANGALIA LIVE NEWS

Sunday, June 28, 2015

MSIBA NEW YORK NA TANZANIA MAZIKO YANATARAJIWA KUWA JUMAPILI JUNE 28,NEW JERSEY,

Familia ya Marehemu Alfred Magege imetangaza mipangilio ya mazishi ya Mzee Alfred Magege siku ya Jumapili, June 28, 
2015 kama ifutavyo: 
10am -Victory SD Church. 
1271 Burke Avenue. 
Bronx. NY 10469
 Funeral service will start promptly 12 noon- 2pm: traveling to 

the Mount Prospect Cemetery, 
2600 Heck avenue,
 Neptune, NJ 07753

 2pm-4pm: Interment Repasse is expected to start at 6pm at Mageges' residence at 2939 Wilson avenue, Bronx, NY 10469
 Tuchangie kupitia www.gofundme.com/wyfewd5


Miriam Abu:9143162814
Seif Akida:9175573195
Buyamba Magege(Son):6469431104
Geoffrey Ngullu:2675826276
Amy Magege:5169467859

15 comments:

Anonymous said...

Huyu Mzee hatujamuona kwenye community ya wa Tanzania wala watoto wake hawajulikani..leo tutoe michango,tutatoa lakini naomba iwe fundisho kwa wale ndugu zetu wasiotaka kujichanganya na wabongo wajichanganye tuwajue..naomba Ibra na Dj Luke irusheni hii comment

Anonymous said...

waheshimiwa tunaomba direction tafadhalini kwa wale wanaotumia usafiri wa wote/public transportation; wasio na gari leo.

Anonymous said...

Chukua treni # 5 Hadi Gun Hill Road. Kutoka hapo ni Dakika 5 tu kwa mguu

Anonymous said...

Wanadiaspora tunapopata Misiba ni Wakati muafaka kujikumbusha mambo mawili.

1. Duniani tunapita je umejiandaaje kiroho??
2. Duniani tunapita je Nikifa LEO familia yangu wataweza kunisitiri nitakavyo? - Bima YA Maisha nimekata?? Jamani WESTADI $300/yr or $25 a month covers your body to either buried in the foreign county or transport back home + 1 ticket for escort of the body + 5 people medical insurance back home including yourself when u visit home UR covered medical. VIONGOZI wa jumuiya Zetu Nadhani ni Wakati muafaka kutoa TAMKO na kuinforce hii insurance Wana diaspora wanunue AU kama una MAKARATASI ZIPO ins mpaka $10 a month. Tumekaa majuu tuonyeshe kuwa tume elimika Maana kuishi huku ni Sawa na Kupata Elimu YA juu... TUBADILIKE.

Anonymous said...

Anon wa juu. "Kuishi huku ni sawa na kupata elimu juu.... wapi na wapi? how do these two things correlate? Kuna waspanish wa ngapi wameishi huku many years na bado hawajaelimika. Haaa? Hata bongo unaweza kupata elimu ya juu. It's good to advocate and encourage people to have life insurance but please don't mix up apples and oranges. VP D.J Luke ule mpango wako wa kuanzinsha funeral/burial account kwa wa diaspora. It's desperately needed naona viongozi wetu wameshindwa kwenye hii issue.

Anonymous said...

inasikitisha tena inasikitisha sana tena sana kabisa.utu wetu na uzalendo wetu uko wapi. naona wanaotoa comment hapa bado ni vijana wadogo au labda ni watu wazima lakini naona wana agenda zao.kwanini tulazimishane kukata bima;kifu kitampata yeyote yule kama huwezi kutoa pesa basi kaa kimya;wana familia unadhani watahisi vipi mnakuja hapa kuwasimanga eti huyu mzee hatumjui wala watoto wake. mweeeee.mweeee. si bure lemutuz anakuchaneni live kila leo na mnamjia juu wakati he is right.
tujiunge na jamii sijui nini na nini,wangapi walikuwa wanajulikana na hii jamii walivyopata shida mbona hakuna hata waliokwenda kuwasaidia ninia mifano kibao.sasa sana tu majigambo na misifa isiyo na mpango.

mnamsimanga maiti na familia yake watu wa aina ghani nyinyi.leo kwao kesho kwenu dunia mapito.
nimesikitika sana kwa comment za hii issue.

mungu aisaidiye sana familia hii na marehemu amen because hakuna kama mungu .

najua dj luke mkuu comment hii hutoweka but message is delivered.

tuwe na moyo wa kupendani na kuoneana huruma especially kwenye msiba tusileta agenda zetu za kujiunga na jumuiya na kuchangia hiyo bima yenu.

Anonymous said...

Sisi Waafrika tuna issue ya kutokubali kuongelea masuala ya vifo. ITS HIGH TIME now dunia imekuwa ndogo watu wanaishi kila mahali ambapo ni mbali na nyumbani. Knowing how much it costs to take the body home from foreign countries then ni wakati muafaka wa kujiandaa mwenyewe ukiwa hai ili wanafamilia wasidhalilike. For one year kumetokea misiba mingapi kila nchi?? Just think about it, tena anza na hapa Marekani. Michango yenyewe si ya pesa za madafu ni dolari $10,000 na kuendelea. Msiba ukiwa DAR unataka kusafirishwa kwenu that was easy ndo maaana si utamaduni wetu kujilipia bima za maisha lakini sasa watanzania tumesambaa duniani tupo maili kibao ukifikwa na mauti unapelekwaje Tanzania. Haya ni maongezi ya kawaida na hakuna mtu anayesimangwa but is the reminder na products hizo zipo huku na hazina usumbufu hata kidogo. You fax death certificate they put money in your account saa hizi mzee wetu angeisha pumzika. JUST THINK POSITIVE... THAN NEGATIVE

Anonymous said...

Point hapo juu madogo wengi na wengine watu wazima zero unaweza ukawa kwenye kujichanganya nao siku ya siku limekukuta wanaunda majungu

Anonymous said...

Ifanyike Harambe. DC kuna watu hawajulikani lakini harambee hufanyika. Tuache kusemana. Tusaidiane ndugu zangu.

Anonymous said...

Watanzania sijui tumerogwa na nani? Wakenya na ukabila wao likija suala la msiba wanakuwa kitu kimoja japo kiukabila. Wabongo ingekuwa hii ni harusi basi wangechanga fasta na kwenda kununua suit za nguvu.
Kama unaona hutachanga wewe piga kimya maana kuna siku na wewe yatakufika na Mungu hulipa hapa hapa duniani.

Anonymous said...

Wewe unayepita kusema kuhusu Bima kwanini usubiri wakati Watu wako kwenye majonzi?kwani usibandike tanzangazo lako kwenye topi c nyingine?kinachoniniudhi kila ukiona tangazo la misiba unakuja kupayuka humu tumechoka.subiri ufiwe halafu weka tangazo hapa.Halafu hata pole husemi.nunua nafasi toa tangazo lako sio katika mud a huu ambao Watu wanamajonzi kuondokewa na baba Yao.kama hutaki changa si tutachanga ndo utamaduni wa mwafrika we Kama mzungu fuata utaratibu wa kizungu.mimi na familia yang u tuna Bima zote unazojua we we lakini kuchanga sitaacha hata iweje.kwanza sio wote wanaenda kuzika Tanzania wengine wanachagua kuzikwa huku ugeninii.acha Roho ya kimaskini mchango wenyewe kwani dolar ngapi mpaka upayuke Kama chiriku hapa.mh Luke usibanie hii huyu mngese asome na mwenzenu anatangaza biashara kwenye misiba ya Watu sio vyema.We wa Bima get a life Lafa.

Anonymous said...

tunagaliye huku na kule kupayuka juu ya bima si fresh but at the same time its a wake up calls,maisha ya ughaibuni kila mmoja wetu anayajua labda kama wewe ni ceo au doctor and lawyer au unakazi mzuri sana na huna shida na mtu unapesa zako mwenyewe ni sawa huto mind mambo ya kuchanga change but kama kabwela kama mimi kama mtu huna bima utachangiwa vipi na wengi ni makabwera kufanya kazi cha kulinda,madukani,na zingine za kubangaiza.tujifunze ndugu zangu hasimwangi mtu wala halazimishwi mtu kuchangia kama hana ila itakuwa poa kama mtu una bima kifo si harusi na hapa si nchi yetu hata kama tuna makaratasi kuna siku utataka upumzike katika udongo wa nchi iliyokulea na kukuzaa mpaka ukaja huku majuu.

bima inasaidia na mnawaondoshea watu kero za kuchanga change si wote wenye uwezo wa kuchanga.ukipeleka kadola kako ka 20 kila mtu atakutole macho wakati ndo uwezo wako huo so kwa nini tunajinyanyasa na kuwanyanyasa watu.

Anonymous said...

watanzania huwa hawachangi bila majungu. kama hutaki majungu nunua bima ya maisha, period! tena hizo bima zitumike wakati tatizo linapotokea maana kuna wa-TZ wana bima na bado wanachangisha

Anonymous said...

Sorry naomba mnisaidie mchango nitakao toa kwenye hiyo link hapo juu utakuwa nakatwa kila mwezi au ni kwa ajili ya msiba huu tu.asanteni

Anonymous said...

Kama hukujiskia kuchangia ungeacha