ANGALIA LIVE NEWS

Monday, June 29, 2015

TPB WACHANGIA DAMU, KUOKOA MAISHA YA WATANZANIA


 Katika kuonyesha kuwa Benki ya Posta Tanzania (TPB), inafanya inatoa huduma za kibenki, lakini pia iko mstari wa mbele kuwajali wateja wake na wananchi kwa ujumla. Katika kutekeleza hilo,  wafanyakazi wa benki hiyo, wakiongozwa na Mkurugenzi Mkuu, Sabasaba Moshingi, wamejitolea damu, "kutunisha" benki ya taifa ya damu na hivyo kuokoa maisha ya watanzania ambapo miongoni mwao ni wateja wake. Zoezi la kutoa damu lilifanyika makao makuu ya benki hiyo barabara ya Samora jijini Dar es Salaam. Pichani Mkurugenzi Mkuu wa benki hiyo, Sabasaba Moshingi, akiwaongoza wafanyakazi wake, katika zoezi hilo.
 Mtaalamu wa masuala ya damu, (kushoto), akimpatia maelezo Meneja Mkuu anayeshughulikia masuala ya kampuni, Norvis Moes, kuhusu utoaji damu
 Moshingi, (kushoto), na mmoja wa wafanyakazi wa TPB, wakitolewa damu kwenye zoezi hilo.

No comments: