ANGALIA LIVE NEWS

Saturday, July 4, 2015

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AKABIDHI ZAWADI ZA WASHINDI WA MASHINDANO YA TANO YA KUHIFADHI QUR-AN TUKUFU YALIYOANDALIWA NA TAASISI YA ISTIQAAMA, JIJINI DAR.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na waumini wa dini ya Kiislamu wakati wa hafla fupi ya Utoaji wa Tuzo na Kuwakirimu washindi wa Mashindano ya Tano ya kuhifadhi Qur-an Tukufu yaliyoandaliwa na Taasisi ya Istiqaama, iliyofanyika kwenye Msikiti wa Istiqaam, Ilala jijini Dar es Salaam jana usiku. Picha na OMR
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkabidhi Cheki ya Sh. Milioni 3, mshindi wa kwanza wa Mashindano ya Tano ya kuhifadhi Qur-an Tukufu, Said Nassor Said, aliyehifadhi Juzuu 30, wakati wa hafla fupi ya Utoaji wa Tuzo na Kuwakirimu washindi hao wa mashindano yaliyoandaliwa na Taasisi ya Istiqaama. Hafla hiyo ilifanyika kwenye Msikiti wa Istiqaama Ilala jijini Dar es Salaam
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na Balozi wa Iran nchini Tanzania, Mehdi Aghajafari, wakati akiondoka kwenye Msikiti wa Istiqaama jana usiku baada ya kushiriki swala ya Talaweh na kukabidhi Tuzo za Kuwakirimu washindi wa Mashindano ya Tano ya kuhifadhi Qur-an Tukufu yaliyoandaliwa na Taasisi ya Istiqaama
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na baadhi ya Waumini wa Dini ya Kiislamu wakati akiondoka kwenye Msikiti wa Istiqaama jana usiku baada ya kushiriki swala ya Talaweh na kukabidhi Tuzo za Kuwakirimu washindi wa Mashindano ya Tano ya kuhifadhi Qur-an Tukufu yaliyoandaliwa na Taasisi ya Istiqaama

2 comments:

Anonymous said...

Alhamdulillah,Alhamdulillah,Alhamdulillah, inafurahisha sana tena sana kuona mnahifadhi quran vijana wadogo;alhamdulillah Allah akuzidishiyeni zaidi na zaidi hapa duniani na kesho akhera.

Na isiwe tu kuhifadhi quran muwe na maadili na muondoko wa quran na kuifuata katika maisha yenu yote hapa duniani.Quran iwe dira yenu kinachokatazwa msikifanye na kinatotaka mkifanye ndo mkifuate kwa sababu ni maneno ya Allah.Na isiwe tu kwa mwezi huu mtukufu wa ramadhan iwe kila siku katika uhai wenu wote muwe mnaisoma,mnaihifadhi na kuifuata,iwe dira yenu ya maisha hapa duniani.

Mashallah nimefurahi sana kuona mnahifadhi quran vijana wadogo wadogo;na tujitahidi sana tuwezi kuihifadhi toka wadogo sana kama watoto wa ki west Africa,nchi kama ivory coast,nigeria,guinne konekri,ghana,mali na kadhalika huwa wana hifadhisha quran watoto wadogo wenye umri wa miaka mitano mpaka tisa anaijua quran yote nzima na tafsiri yake yote na wana kuwa na maadili ya ki QURAN.wengi wa wazazi wao wanajitahidi kulifanya hili jambo hata wakiwa majuu.na ndo maana tunaona na tamaduni zao huwa hawaziachi.

Allah akujaliyeni kila la kheir waislamu wote na kizazi chenu chote na umma wote wa kiislamu katika mwenye huu wa rehma tuwe tunapendana na kutendeana wema na kuoneana huruma kwa siku zote. na pia kuwaonea huruma binadamu wenzetu wasio katika dini yetu.Amin ya rabbal alamin.

DJ LUKE NA VIJIMAMBO TEAM WOTE NATOA SHUKRAN SANA KWA NIAMBA YANGU NA WAISLAMU WOTE KWA KUTUWEKEA MATUKIO YA DINI YENU.MUNGU AKULIPENI KILA LA KHEIR NA LENYE SHARI AKUEPUSHIYENI NALO.MUNGU PEKE NDO ATAKAYE KULIPENI KWA WEMA WENU.AMIN YA RABBAL ALLAMIN.

AHSANTE SANA DJ LUKE,IBRA NA VIJIMAMBO TEAM WOTE AHSANTENI SANA SANA KABISA.

Anonymous said...

nimefurahi sana kuona comment yangu umeiweka hapo juu ahsante sana sana kabisa vijimambo team wote.Mungu akubarikini sana.ameen