ANGALIA LIVE NEWS

Friday, July 10, 2015

MHE. BALOZI LIBERATA MULAMULA , KATIBU MKUU WA WIZARA YA MAMBO YA NJE NA USHIRIKIANO WA KIMATAIFA AWASILI JIJINI WASHINGTON DC.


Mhe.Balozi Liberata Mulamula, Katiba mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na ambaye ni Balozi wa Tanzania nchini Marekani awasili jijini Washington DC na kulakiwa na wafanyakazi wa Ubalozi, pichani ni afisa Swahiba Habib Mndeme akikabidhi maua mara tu baada ya Mheshimiwa kuwasili.
Mhe, Balozi Liberata Mulamula mwenye furaha baada ya kulakiwa na afisa Swahiba Mndeme.
 
Mhe, Balozi Liberata Mulamula akiwa na Mkuu wa Utawala Bi. Lily Munanka pamoja na Mwambata wa Jeshi Col. Adolph Mutta mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Dulles.
Zawadi ya maua na kadi maalum kwa ajili ya Mhe. Balozi iliyoandaliwa na wafanyakazi wa Ubalozi wa Tanzania Washington DC.
Mhe, Balozi Liberata Mulamula akisoma kadi ya pongezi iliyotolewa maalum kwa ajili yake.
Mhe,Balozi Liberata Mulamula akiwa nyumbani kwake Bethesda ,Maryland mara baada ya kuwasili.
Mhe, Balozi Liberata Mulamula kwenye picha ya pamoja na baadhi ya maafisa na wafanyakazi wa Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani mara tu baada ya kuwasili nyumbani kwake Bethesda, Maryland.

PICHA ZOTE KWA HISANI YA CAMERA YA UBALOZI.

No comments: