ANGALIA LIVE NEWS

Saturday, July 4, 2015

STARS NA UGANDA ZATOKA SARE 1-1 NAKIVUBO


Na Baraka Kizuguto, KAMPALA
TANZANIA imetupwa nje ya michuano ya Ubingwa wa Mataifa ya Afrika (CHAN) baada ya sare ya 1-1 jioni ya leo Uwanja wa Nakivubo, Kampala, Uganda.
Matokeo hayo yanamaanisha, Stars imetolewa kwa kipigo cha jumla cha mabao 4-1, baada ya awali kufungwa 3-0 katika mchezo wa kwanza wa Raundi hiyo ya kwanza visiwani Zanzibar wiki mbili zilizopita.
Dakika 45 za kwanza zilimalizika kukiwa hakuna timu iliyopata bao na kipindi cha pili na kipindi cha pili, John Bocco ‘Adebayor’ alianza kuifungia Tanzania kwa penalti dakika ya 53 kwa penalti.


Kikosi cha Taifa Stars kilichotoa sare ya 1-1 na Uganda leo Kampala
Penalti hiyo ilitolewa baada ya beki wa Uganda kuunawa mpira uliopigwa na mshambuliaji wa Tanzania, Rashid Mandawa.
Uganda walifanikiwa kupata bao la kusawazisha dakika ya 82, kupitia kwa Kizito Hezron na wanasonga mbele katika mbio za CHAN ya mwakani nchini Rwanda. 
Matokeo haya ya sare baada ya vipigo vitano mfululizo kwa Stars yanakuja chini ya kocha mpya, Charles Boniface Mkwasa kufuatia kufukuzwa kwa Mholanzi, Mart Nooij baada ya kufungwa na Uganda 3-0 Zanzibar.
Kikosi cha Uganda kilikuwa; James Alitho, Muzamiru Mutyaba, Brian Ochwo, Hassan Waswa, Denis Oola, Faruk Miya, John Shemazi/Robert Sentongo, Bakaki Shafik, Tekkwo Derick/Kizito Hezron/Kalanda Frank.
Tanzania; Ally Mustafa ‘Barthez’, Shomary Kapombe, Mwinyi Hajji Mngwali, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, Kevin Yondan, Mudathir Yahya, Deus Kaseke, Frank Domayo/Said Ndemla, John Bocco, Rashidi Mandawa na Simoni Msuva/Ramadhani Singano ‘Messi’.

No comments: