Afisa Masoko Bi. Kilave Atenaka (Kulia) wa Taasisi ya Miradi na Maendeleo ya Miundo Mbinu iliyochini ya Wizara ya Fedha (UTT –PID) akiwasikiliza wateja waliotembelea katika banda kwenye maonyesho ya 39 ya Biashara ya Kimataifa, Dar es Salaam yanayoendelea katika mabanda ya Saba Saba katika Viwanja vya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere ndani ya banda la Wizara ya Fedha.
Afisa Masoko Bi. Kilave Atenaka (Kushoto) wa Taasisi ya Miradi na Maendeleo ya Miundo Mbinu iliyochini ya Wizara ya Fedha (UTT –PID) wakiwa na nyuso za furaha na Bi. Beatrice Ngoda katika banda kwenye maonyesho ya 39 ya Biashara ya Kimataifa, Dar es Salaam yanayoendelea katika mabanda ya Saba Saba katika Viwanja vya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere ndani ya banda la Wizara ya Fedha.
Afisa Masoko Bi. Mary Minja (Kulia) wa Taasisi ya Miradi na Maendeleo ya Miundo Mbinu iliyochini ya Wizara ya Fedha (UTT –PID) akimsikiliza mteja aliyetembelea katika banda kwenye maonyesho ya 39 ya Biashara ya Kimataifa, Dar es Salaam yanayoendelea katika mabanda ya Saba Saba katika Viwanja vya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere ndani ya banda la Wizara ya Fedha.
Taasisi ya Miradi na Maendeleo ya Miundo Mbinu iliyochini ya Wizara ya Fedha (UTT –PID) ipo kwenye maonyesho ya 39 ya Biashara ya Kimataifa, Dar es Salaam yananoendelea katika mabanda ya Saba Saba katika Viwanja vya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.
Banda la UTT PID lipo jirani na kuingia katika Banda la Wizara ya Fedha upande wa kulia… karibuni sana wananchi mnaombwa kujitokeza kwa wingi mjipatie huduma mbali mbali zinazotolewa na taasisi hiyo ikiwemo huduma za uuzwaji wa viwanja katika maeneo mengi ya nchi ikiwemo vile vya mradi wa katika Taasisi ya Miradi na Maendeleo ya Miundo Mbinu iliyochini ya Wizara ya Fedha (UTT–PID) miji ya Chalinze na Bagamoyo mkoani Pwani.
Akielezea Afisa Masoko Bi. Kilave Atenaka alisema kuwa kwa sasa wanaendesha huduma ya uuzwaji wa Fomu kwa ajili ya Viwanja, pia wanatarajia kuanza kuuza kwa umaa na taasisi mbali mbali miradi mipya ikiwemo wa Tundwi Songai – Kigamboni jijini Dar es Salaam na ule wa Kingorwila, Morogoro.
Aidha Bi. Kilave alitumia wito huo kuhamasisha wananchi kujitokeza kwa wingi ndani ya banda hilo kujipatia elimu mbali mbali zitolewazo na taasisi hiyo hapa nchini.
Kwa sasa UTT PID ni miongoni mwa taasisi zinazofanya vizuri katika utoaji huduma za ushauri katika maeneo ya upembuaji yakinifu wa miradi mbali mbali, uratibu wa fedha na huduma zinazohusian katika maandalizi ya mapendekezo ya miradi kwa benki au taasisi za fedha, uteuzi wa watoa huduma kuhusiana na maandalizi y a zabuni na usimamizi wa majengo na mali ambao ni utoaji wa huduma fanisi za usimizi wa majengo yaliyochini ya uangalizi thabiti wa taasisi.
No comments:
Post a Comment