ANGALIA LIVE NEWS

Friday, July 3, 2015

Wastara: Nimeamua Kumpa Bond Nafasi ya Kunioa, Mimi Bado Damu Changa Nikisema Siwezi Kuolewa Tena Najidanganya..Nimempa Bond Sharti Hili...


Wastara na Bond Mapenzini
Brighton Masalu

WASTARA Juma Issa Abeid amekiri kuzidiwa na hisia za kuwa na mwenza kutokana na ukweli kwamba damu yake bado changa, hivyo suala la kuolewa halikwepeki huku akimpa nafasi kubwa msanii mwenzake, Bond Bin Sinan endapo atakidhi vigezo na masharti.
Akifungulia ‘koki’ ya maneno mbele ya paparazi wetu kwa njia ya simu mwanzoni mwa wiki hii, Wastara ambaye kwa sasa yuko bize kusaka ubunge nyumbani kwao Morogoro Vijijini, alisema hawezi kudanganya kwamba ataishi bila kuwa na mume kwa kuwa amekamilika kimaumbile.

Wastara na Bond Katika Pozi

“Mimi ni mwanamke, nimekamilika tena nakula na ninashiba. Damu bado changa. Nikisema siwezi kuolewa, nitakuwa nadanganya. Nimekaa muda mrefu kwa sababu kila mwanaume anayenihitaji ananitamani tu.

“Bond namuona ni mwelewa. Lakini nimempa sharti la kutonigusa hadi siku ya ndoa. Kama atakidhi na hayo mengine ambayo ni siri yetu, niko tayari kuolewa naye,” alisema Wastara.
GPL

2 comments:

Anonymous said...

Sadakta mummy umenena kweli tupu na sharti lako ni la kweli lakini kitu kidogo tu angali,je anakufuaa kwa ajill ghani isije ikawa kwa pesa zako wanawake wengi huwa mwanamme anamfuata kwa hilo na especially akimuona hana mchungaji(mume).

na je watoto wako amewakubali angalia hilo pia. na cha muhimu kuliko chote kaa usali salaatu istighar ni salaa ya kumuomba mungu akuonyeshe kama ana kweli kheiri na wewe huyu james bond wako.

kama huijui kuisali hii salaa mtafute mtu akufundishe au google. na mungu atakuotesha au ataufanya moyo wako kuwa mwepesi na utamkubali au kuwa mzito na utamkataa.

mungu ndo kila kitu kutafuta ushauri kwake hajalishi damu change unakula ukashiba ukahara yeye ndo aliyekuumba na yeye peke ndo anayejua mahitaji yako.

so muweka mungu mbele na sali salaa hiyo ndo muhimu kuliko yote;kuliko hata feelings zako zakumpenda james bond wako.

ushauri wa bure tu dada yangu wastara na Allah inshallah atakustiri.amen

ramadhan kareem/Mubarak na wadau wote popote pale mlipo ramadhan kareem.

dj pia na wewe ramadhan kareem ha ha ha.

Anonymous said...

.majina kama haya siku hizi hayapo ni mazuri sana majina ya kimila.wastaraa hasumbuki jina lako zuri mashallah kama wewe mwenyewe.usijali utastirika tu;na aliye mkweli kama wewe mwenyewe.