ANGALIA LIVE NEWS

Thursday, August 6, 2015

Hayati Mwalim Nyerere akimzungumzia kukataliwa kwa Edward Lowassa katika...

12 comments:

Anonymous said...

Thats 20 some yrs ago....so kila mtu alishindwa kupata anacjotafuta yrs ago ubaki hivyo hivyo...mbona JK alikatwa na mwalimu but amekuja kuwa raisi.....achenj ujinga CCM ya enzi zile siyo ya sasa and time has changed .....mtashindwa mwaka huu

Anonymous said...

Haina mantili yeyote ile katika nyakati hizi mwalimu alishaondoka tunaangalia mateso na maisha ya mwelekeo mzima wa waTanzania ambao yeye mwenyewe alituanzishia yote haya. Hatarudi hata tumtangaze milele. Tusonge mbele.!!

Anonymous said...

Jamani mtu kutoa maoni yake ni haki yake lakini wengine naona kama akili zao zimeoza kwa hivyo hata hayo maoni yao yameoza . Kuna watu duniani wanaitwa ( smart people) watu ambao uweledi wao wa mambo upo tofauti na watu wa kawaida .Nyerere hapana shaka ni mingoni mwa hao watu kama unabisha basi utakuwa unaifuraisha nafsi yako lakini ukweli unabakia pale pale. Yaani mtu anathubutu kufikiri ati miaka 20 ni muda uliopitwa na wakati? sasa wamarekani miaka mia mitatu iliopita ni kama jana , George Washington, Abraham Lincoln na viongozi wengi wa zamani mawazo yao ni misingi walio iweka inaishi katika maisha ya kila siku ya wamerekani . Na si marekani tu nchi zote hizo tunazozitamani misingi ya wazee wao wa zamani ndio inawaongoza. Ati haina mantiki yoyote?
Kama hamna cha kusema acheni kuropokwa. Ikowapi Libya, iko wapi, Iraqi, iko wapi Nigeria, ikowapi,Egypt, ikowapi south Africa tumeona jinsi walivyo waua waafrica wenzao ni kiasi gani wamesahu junsi Mandela alivyowasihi kuhusu kuvumiliana. Mwalimu alishamuona lowasa zamani sana kuwa ni mtu asiefaa kuwa kiongozi wa nchi.

Anonymous said...

Wewe mdau watatu hapo juu ndio hauna maana kabisa, unasema mwalimu alishamuona Lowasa hafai kwani yeye alikuwa Mungu. Kama angekuwa smart asingetuweka kwenye ujamaa angalia sasa hatujui hata tuko kwenye mfumo gani. Labda useme mfumo usio na kichwa wala miguu, nyuma wala mbele , juu au chini tunaenda tuu kama hatuna vichwaa

Anonymous said...

Mwalimu aliona mbali sana, aliyasema yote hayo kabla ya Richmond kutokea. Sasa tumeshuhudia ufisadi papa katika Richmond na mengine mengi sana, yote haya yatafanya safari ya matumaini iishie kuwafuata akina Mramba na Yona Keko.

Lipumba na Slaa nao wametuthibitishia kuwa wao ni viongozi makini, mwenye maadili mema na nia thabiti ya kumkomboa mtanzania. Wamekataa kula matapishi yao kwa kununuliwa na fisadi papa Edward Lowassa, ambaye walimtaja sana kwenye hotuba zao. Tofauti na akina Mbowe, Seif Sharif, Mbatia, Makaidi na akina Lissu, kwao wao HAPENDWI MTU ILA POCHI. Wamesahau kabisa nafasi yao katika jamii, kwamba Lowassa na sera zake ni kinyume kabisa mitazamo yao. Sasa kwa njaa zao wamekubali kula matapishi yao, kweli bongo hakuna upinzani.

Jambo ambalo tunatakiwa kulifahamu ni kuwa, hata kama CCM wakiamua wasimfunge jela Lowassa, bado hana ubavu wowote wa kupambana na Magufuli.

Anonymous said...

Mdau wa nne hapo juu @11:32PM yaelekea hujasoma na kama umesoma, basi hujaelimika. Tanzania inayo historia ya kipekee Afrika kwa sababu ya hayati Mwalimu Nyerere. Kupitia ujamaa aliweza kuiweka nchi kuwa ya Amani na utulivu. Nchi yetu imekuwa na umoja licha ya kuwa na makabila 120. Niambie nchi gani nyingine Afrika ambayo imekuwa shwari bila vita vya wenyewe kwa wenyewe? Tazama Nigeria, Kenya, Rwanda, Uganda, Ethiopia, Burundi,n.k.,ambako ukabila umemwagisha damu za maelfu ya raia zao. Hizo hazikuwa nchi zenye siasa ya ujamaa; and for your information nimezitembelea hizo zote, and they are not that better-off economically than Tanzania; and in facts, in most of these countries, the gap between the rich few is bigger than the poor majority. Acha siasa ya ushabiki, you need facts at hand kabla ya kutoa commentaries za kitoto. Elimu haina mwisho mdau, you still have time to learn, regardless of your age.

Anonymous said...

Mwalimu alikuwa ni mtu wa pekee!alikuwa na uwezo wa kujua ya nbele kwani mengi tunayaona wazi wazi! Kila mtu anahaki ya kusema chochote kwa upeo alionao,binfsi naona tuyaonayo ni maono ya mwalimu ya muda mrefu.

Anonymous said...

Mm najua watanazania wana taka mini, hawataki kua na maisha mazuri, wanataka kila mtu awe na pesa ya kushinda bar kua na vimada 6 sio kua na serkali nzuri itakayo boresha elimu,afya,usafiri , kila mtu anafikiria yupi mzuri akingia ikulu itakua rahisi kuiba, julias aliwajua wote mapema

Anonymous said...

Mbona CCM hawayafanyii kazi mambo yote aliyowahi kuyasema..Nyerere si alikataza ubinafisishaji wa viwanda?ccm ikabinafisisha yote..Nyerere alikataa kuuzwa kwa NBC..ccm ikaiuza NBC kwa bei ya bure...Nyerere alikataza viongozi kufanya biashara...viongozi almost wote wa CCM ni wafanyabiashara!..kuna mambo mengi Nyerere alikataza lakini CCM imeyafanya na wakiulizwa huwa wanasema hizi ni zama nyingine. Na katika HILI pia JIBU NI HII NI ZAMA NYINGINE...go go Lowassa go go gooo UKAWA.

Mdau
sweden

Anonymous said...

Wa-tz amkeni sasa hivi ni wakati adimu sana katika maisha yenu kuliko wakati mwingine. Hii ndio nafasi ya pekee kabisa katika maisha ya wengi hapo tanzania. Mkikosea na kuichagua CCM mjue hamtaweza tena kuitoa madarakani mpaka miaka kumi ipite which will be too late. Yaani kama mtu ukitafakari kwa kina umaskini ulipo tz na matanuzi wanayofanya CCM hutafanya makosa kwenye kupiga kura.

Wa-tz maskini tafakarini sana huu mfumo kwa miaka zaidi ya 50 umewafanya maskini wa kutupwa. Tz kuna watu wachache wana maisha mazuri kupitia huu mfumo..ni wachache sana..angalieni wa-tz maskini msije kudanganywa na hawa watu wachache mkaendelea kuteseka kwa miaka mingi mingine. Itasikitisha sana wewe raia maskini kuichagua CCM halafu baada ya uchaguzi kuendelea kulalamika kuwa maji, umeme, huduma za hospitali ni shida. Hakuna atakae kuonea huruma na hakuna atakae kusikiliza. Mtanzania maskini tafakari umaskini wako na wa familia yako kwa kina halafu ndipo uende kupiga kura.

mdau
UK

Anonymous said...

Watanzania muwe basi na uwezo wa kufikiri. Wewe kutembelea nchi hizo sasa unamweleza nani??? Watu wote wenye mitabia ya kujitapa tapa wanasema kama wewe unavyosema.....eti umefika huko kote? Kwani kufika huko ni sababu?? Je ungetembea dunia nzima mbona tungekoma? Kaka uwezo wa ku-analyze mambo si lazima ufike Kenya, Nigeria, Rufiji N.k . Msimweke Nyerere kuwa kipimo kwa kila kitu...siyo kila anachosema au kufikiri ni sahihi...au ndiyo yale ya Kidumu fikra sahihi za mwenyekiti wa CCM? Leo tunaonekana majuha kwa kutukuza watu, ndiyo maana inakuwa shida sana kwa wale waliopo kwenye uongozi kujiuulu na kuwaachia wengine kwa sababu tumeaminishwa kuwa kuna watu wamezaliwa kuwa viongozi na wengine watawaliwa hivyo tumejijengea matabaka...tukielimishwa tunakataa tunajifanya tumetembelea nchi za ajabu ajabu lakini tunashindwa kupambanua nini ni nini. Hamsemi kwa nini nchi nyingine hazipigani reference zenu ni kwa nchi za Africa zilizokomaa kwa ukabila.

Anonymous said...

Nonsense! Sijui ni utaahira wa aina gani huu kufikiria kwamba wachezaji wabovu waliokuwa wachezaji wa CCM watakuwa wachezaji nyota ndani ya UKAWA! Can't you use your brain for a second?