Tuesday, August 18, 2015

JUMUIYA YA QAMER YA CANADA PAMOJA NA JUMUIYA YA TAQWA TANZANIA YATOA MISAADA PEMBA

VITANDA mbali mbali vya Hospitali vilivyotolewa na Jumuiya ya Qamer Foundation ya nchini Canada, ikishirikiana na Jumuiya ya TAQWA Tanzania, kwa ajili ya Hospitali Kisiwani Pemba kabla ya kukabidhiwa kwa uongozi wa Wizara ya Afya Pemba.
MABOKSI mbali mbali yenye madawa kwa ajili ya Hospitali pamoja na mikoba ya Watoto mayatima, vilivyotolewa na Jumuiya ya Qamer Foundation ya nchini Canada, ikishirikiana na Jumuiya ya TAQWA Tanzania, mikoba kwa aajili ya wanafunzi wa skuli.
WANANCHI mbali mbali wakiangalia Vitanda, Boksi za madawa, baskeli za walemavu,Magongo ya watu wenye ulemavu, pamoja na Standi za kutundukia dripu, Vilivyotolewa na Jumuiya ya Qamer Foundation ya Nchini Canada, ikishirikiana na Jumuya ya TAQWA Tanzania.
WANANCHI mbali mbali wa jimbo la Ole na shehia jirani, wakiwasikiliza kwa makini viongozi mbali mbali wa Serikali na Jumuiya ya TAQWA Tanzania pamoja na Qamer Foundation ya Nchini Canada, kabla ya kukabidhiwa kwa vifaa hivyo kwa wananchi hao.
WAZIRI wa Katiba na Sheria wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na Mwakilishi wa Jimbo la Mgogoni Pemba, Aboubakar Khamis Bakar wa pili kushoto akiwa na mwakilishi wa jimbo la Ole Hamad Massoud Hamad, pamoja na viongozi wa Jumuiya ya TAQWA Tanzania na Jumuiya ya Qamer Foundation ya Nchini Canada.
MWAKILISHI wa Jimbo la Ole kisiwani Pemba Hamad Masoud Hamad, akizungumza katika hafla ya kukabidhi vifaa mbali mbali ikiwemo Vitanda vya Hospitali, vigari vya walemavu, mikoba ya skuli huko Ole kisiwani Pemba.
WAZIRI wa Katiba na Sheria wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na mwakilishi wa Jimbo la Mgogoni Kisiwani Pemba, Aboubakar Khamis Bakar, akizungumza katika hafla ya kukabidhi vifaa mbali mbali ikiwemo Vitanda vya Hospitali, vigari vya walemavu, mikoba ya skuli huko Ole kisiwani Pemba.
MKURUGENZI mtendaji wa Jumuiya ya TAQWA Tanzania Dk.Salha Mohamed Kassim, akizungumza katika hafla ya kukabidhi vifaa mbali mbali ikiwemo Vitanda vya Hospitali, vigari vya walemavu, mikoba ya skuli huko Ole kisiwani Pemba.
Mkurugenzi Mkuu mtendaji wa Jumuiya ya Qamer Foundation kutoka Canada Balkis Alhadad, akizungumza katika hafla ya kukabidhi vifaa mbali mbali ikiwemo Vitanda vya Hospitali, vigari vya walemavu, mikoba ya skuli huko Ole kisiwani Pemba.
BAADHI ya wanachama wa Jumuiya ya Qamer Foundation kutoka Canada, wakimvisha mkoba wa skuli mtoto yatima, ambae ni mwanachama wa jumuiya y tahafidh Quran na Maendeleo ya Kiislamu ya Jimbo la Ole.
BAADHI ya wanachama wa Jumuiya ya Qamer Foundation kutoka Canada, wakiwakabidhi viongozi wa Wizara ya Afya Pemba, Magodoro na vitanda kwa ajili ya Hospitali hafla hiyo ya makabidhiano iliyofanyika huko katika skuli ya Ole kisiwani Pemba.
AFISA Mdhamini Ofisi ya Makamo wa kwanza wa Rais wa Zanzibar, Fatma Mohamed Omar, akipokea msaada wa vibaskeli kwa ajili ya watoto wenye ulemavu, vilivyotolewa na Jumuiya ya Qamer Foundation kutoka Canada.(Picha na Hanifa Salum, PEMBA.)

No comments: