Afisa Mawasiliano wa Kampuni ya Kuendeleza Jotoardhi Tanzania (TGDC) Bi. Johari Kachwamba akiwaelimisha Viongozi wa Kata ya Mwasanga na Tembela kuhusu majukumu ya TGDC leo 7 Agosti, 2015 Mkoani Mbeya.
Mhandisi Mwandamizi toka Wizara ya Nishati na Madini, Bwana. Jacob Mayalla akiwaelimisha Viongozi wa Kata ya Mwasanga na Tembela kuhusu historia ya tafiti za jotoardhi kwa mkoa wa Mbeya leo 7 Agosti, 2015 Mkoani Mbeya.
Baadhi ya Viongozi wa Kata ya Mwasanga na Tembela wakifuatilia kwa makini elimu ikiyotolewa na Wayendaji wa TGDC leo 7 Agosti, 2015 Mkoani Mbeya.
PICHA ZOTE NA BENEDICT LIWENGA.
NA BENEDICT LIWENGA, MAELEZO, MBEYA.
Nishati ya jotoardhi imeelezwa kuwa ni nishati usiyokuwa na kikomo kwani pindi inapovunwa huwa haiishi na matumizi yake yanakuwa endelevu kwasababu pindi mvuke unapopatikana toka katika maji ya jotoardhi, maji yake hutumiwa kwa shughuli za moja kwa moja ikiwemo ukaishaji wa mazao, uzalishaji samaki ikiwemo na utalii.
Hayo yameelezwa leo na Mhandisi Mwandamizi toka Wizara ya Nishati na Madini, Bwana Jacob Mayalla wakati Timu ya Shirika la Uendelezaji wa Nishati ya Jotoardhi Tanzania (TGDC) ikiendelea na kampeni yake ya kuelimisha viongozi pamoja na wanavijiji kuhusu faida ya jotoardhi nchini.
Mayalla amesema kuwa utafiti kuhusu upatikanaji wa jotoardhi ulianza miaka ya nyuma ya 1976 hadi 1978 ambapo mkoa wa Mbeya umekuwa miongoni mwa mikoa ambayo jotoardhi inasemekana ipo kutokana na tafiti hizo.
"Mkoa wa Mbeya ni miongoni mwa mikoa iliyobarikiwa kuwa na jotoardhi, hivyo Serikali kupitia Kampuni hii ya TGDC inakusudia kuanza shughuli za upimaji ili kuweza kupata nishati hii na kuweza kutatua changamoto za upatikanaji wa umeme katika mkoa huu", alisema Mayalla.
Akitaja baadhi ya matumizi ya moja kwa moja, Mhandisi Mipango toka TGDC, Bwana Chagaka Kalimbia ameeleza kuwa, jotoardhi ina matumizi mbalimbali ikiwemo kupadha nyumba joto, kuzalisha mazao ya mbogamboga kwa kutumia Vitalu Nyumba, vyanzo vya kitalii kwa nchi pamoja na matumixi mengineyo ambayo yanapelekea kuongeza vipato vya wananchi na taifa kwa ujumla.
"Mradi huu una manufaa kwa wananchi kwa mfano kwa mkoa wa Mbeya ambao kuna baridi kali, jotoardhi inaweza kutatua changamoto hii kwa kutengeneza miundombinu ambayo itasaidia kupasha nyumba joto, lakini pia kwasababu mkoa huu unategemea kilimo, basi jotoardhi hii itakuwa mkombozi kwa uzalishaji mkubwa wa mazao mbalimbalu kwa kukaushia maxso yao kwani nishati ya jua katika maeneo haya siyo ya uhakika".
Naye Afisa Mawasiliano wa TGDC, Bi. Johari Kachwamba ameeleza mandhari nzima wa madhumuni ya TGDC kwa wananchi na kwa Taifa zima ikiwemo hali ya uzalishaji wa umeme hapa nchini, historia ya TGDC, Dira na dhamira kuu ya TGDC ili kuifanya jamii ipate uelewa mzuri kuhusu majukumu ya Kampuni hiyo.
Kwa upande wake Afisa Sayansi ya Jamii, Bi. Eva Nyantori ameeleza masuala mbalimbali kuhusu namna gani jamii inashitikishwa na mradi huo kwa manufaa ya wananchi hususani fursa mbalimbali ambazo jamii inatarajiwa kuzipata zikiwemo fursa za ajira ambazo huleta kipato hali ambayo inapelekea uchumi wa eneo kukua kwa kasi kutokana na na nishati hiyo.
"Jamii itarajie kupata fursa mbalimbali mfano sekta za barabara, ajira kwa wananchi, kodi itokanayo na mradi huo, upatikanaji wa umeme wa nafuu kwa wakazi wa eneo husika, hivyo ni matumaini yetu kuwa nishati hii itapunguza gharama kwa wananchi wa mkoa huu", alisema Nyantori.
Akizitaja changamoto za mradi huo, amesema kuwa kuna Sheria namba 4 na 5 ya 1999 ili kuweza kufanya fidia kwa maeneo yayaksyohusika na mradi ambapo Sheria hiyo inaitaka kufanya fidia hiyo ndani ya miezi Sita kabla ya mradi huo kuanza rasmi kuchimbwa, lakini elimu kuhusu fidia hiyo itatolewa ili kumfanya mwananchi apate kuelewa.
TGDC inatarajia kuzalisha zaidi ya Megawati 200 za nishati ya umeme kwa mkoa wa Mbeya ambao utatokana na nishati ya jotoardhi ambapo kwa sasa mkoa huo unatumia Megawati 40.
No comments:
Post a Comment