Mtangaza nia ya kuwania nafasi ya Urais wa Tanzania kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Waziri Mkuu Mstaafu, Mh. Edward Lowassa akiwapungia maelfu ya wafuasi na wapenzi wa Chama hicho, wakati alipowasili kwenye Ofisi ya Makao Makuu ya Chama hicho, Kinondoni Jijini Dar es Salaam. Mh. Lowassa alifika ofisini hapo kurudisha fomu za kuomba ridhaa ya Chama hicho, kuwania Urais kwenye Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 25 mwaka huu.
Mtangaza nia ya kuwania nafasi ya Urais wa Tanzania kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Waziri Mkuu Mstaafu, Mh. Edward Lowassa akiwasalimia wafuasi wa Chama hiyo kwa ishara ya vidole viwili.
Makamu Mwenyekiti wa Chadema, Profesa Abdallah Safari (kushoto) akipokea fomu kutoka kwa Waziri Mkuu wa Zamani, Edward Lowassa
Ester Bulaya (wa kwanza kushoto waliovaa fulana) akiwa ukumbini kumshuhudia Edward Lowassa akirudisha fomu ya kugombea urais ndani ya chama.
Baaadhi ya mabango yaliyokuwa yamebebwa na wanachadema
No comments:
Post a Comment