ANGALIA LIVE NEWS

Wednesday, August 5, 2015

PICHA ZA UFUNGUZI WA MAONYESHO YA NANENANE NA UFUNGUZI WA MAADHIMISHO YA WIKI YA UNYONYESHAJI KITAIFA INAYOFANYIKA MKOANI DODOMA

 Wanafunzi wa shule ya msingi ya  Nhinhi wiyani Chamwino wakicheza ngoma ya kabila la kigogo wakati wa Uzinduzi wa maadhimisho ya siku ya Unyonyeshaji maziwa ya mama kwa mtoto kwa miezi sita yaliyofanyika katika kijiji cha Nghwenda katika mfurulizo wa wiki ya hiyo inayofanyika kitaifa mkoani Dodoma


 Baadhi ya wanawake na wanaume wakiwa na watoto wao kwenye uzinduzi wa maadhimisho ya wiki ya Unyonyeshaji kitaifa inayoendelea mkoani Dodoma yaliyofanyika katika kijiji cha Nghwenda kata ya Nhinhi wilayani Chamwino.
 
Nahodha wa Timu ya mpira wa miguu ya Watoto wa Town ya kijiji cha Nhinhi Babuu Abel akipokea zawadi ya Mpira toka kwa Katibu Tawala wa mkoa wa Dodoma Rehema Madenge baada ya timu yake kushika nafasi ya pili kwenye mchezo wa fainali wa maadhimisho ya siku ya unyonyeshaji ambapo nafasi ya kwanza ilienda kwa Small Boys iliyopata zawadi ya Jezi.

 Mtoto Mwenye umri wa miaka saba akingoza kikundi cha nyota katika upigaji na uchezaji wa ngoma wakati kikundi hicho kilipokuwa kikiwatumbuiza wakili, wafugaji na watu mbalimbali wanaohudhuria maonyesho ya Nanenane yanayoendelea kikanda mkoani Dodoma kabla ya Mkuu wa mkoa huo kuyafungua Rasmi maonyesho hayo.

  Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Chiku Gallawa, akiangalia mazao aina ya Uwele ambayo inashauriwa kulimwa kwa wingi katika mikoa ya kanda ya kati kutokana na mazao hayo kustahimili ukame.
 Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Luteni Mstaafu Chiku Gallawa akiangalia Nyanya aina ya NOR F1 zilizopo katika banda la wilaya ya Kondoa, zinazolimwa na Clabu ya vijana wa vyuo vikuu kabla ya kufungua  maonyesho ya Nane hapo jana.
 Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Chiku Gallawa akipokea Nyanya aina ya NOR FI toka kwa Mkuu wa kitengo cha mafunzo ya kilimo cha kisasa wa Clabu ya Vijana wasomi wa Elimu ya juu Agrikolas Masigati wakati mkuu huyo wa moa alipotembelea Banda la maonyesho la Wilaya ya Kondoa katika viwanja vya maonyesho ya nanenane jana.

 Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Chiku Gallawa akionyeshwa mashine ya Kutotolesha Vifaranga kwa siku kumi na tano na Mjasriamali Dicky Mushi  kwenye Banda la maonyesho la wilaya ya Singida katika viwanja vya nanenane.

 Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Chiku Gallawa akiangalia Mnyama Sokwe na Ndege aina ya Tai waliokaushwa kwenye mabanda ya Maliasili na Utalii jana alipotembelea na kujionea wanyama wa aina mbalimbali akiwemo kobe aliishi kwa zaidi ya miaka mbali, Aliambatana nae ni Mkurugenzi wa maliasili na Utalii Uzeeli Kiangi.

No comments: