Tuesday, August 18, 2015

SHUKURANI ZA DHATI

Ebra NY akiwa JFK kuelekea Tanzania kuhani msiba wa mpendwa dada yake Asha Nyagaly aliyefariki siku ya Jumamosi Aug 15. 2015 Tanzania.

Familia ya Nyagaly inapenda kutoka shukurani zake za dhati kwa Jumuiya ya Watanzania New York New Jersey,Connecticut na Pennsylvania kwa ushirikiano mliotoa kwa kumfariji mtoto wao Ebra Ny na familia kwa ujumla kusema kweli Ebra na familia wamefarijika sana hasa katika kipindi hiki kigumu cha kuondokewa na mpendwa wetu Asha Nyagaly, Pamoja na kwamba taarifa ya msiba ilitolewa siku ya Jumamosi na Ebra alikua aondoke siku ya Jumapili kuelekea Tanzania wanajumuiya waliojitokeza nyumbani kwake kumpa pole walikua ni wengi kusema ukweli tumefarijika sana m umoja wenu ni mfano wa kuigwa na jumuiya zingine. Kuna ambao walipiga simu kutoka majimbo mbalimbali na wengine kupiga kutoka nchi za ng'ambo yote ni katika kumfariji Ebra Ny katika msiba huu wa mpendwa dada yake.

Shukurani za pekee kwa . Ubalozi na Wafanyakazi wa Ubalozi wa Tanzania Umoja wa Mataifa New York, Dr Temba, Mwenyekiti wa Jumuiya ya Watanzania New York,akina dada wa hiari wa Ebra New York kwa kujitolea tangia kufanya maandalizi ya ununuzi wa vyakula na kupikia wageni waliofika kumfariji mtoto wetu Ebra Nyagaly siku hiyo ya Jumamosi, wachezaji wa timu ya mpira ya New York na wale wote walioshiriki kwa njia moja au nyingine na kumfariji Ebra Nyagaly katika kuwezesha na kufanikisha safari yake Tanzania.

Kama kutakua kuna yeyote amesahaulika tunaomba radhi kwani si kusudio letu kufanya hivyo.

Hatuna cha kuwalipa kitakacholingana na haya yote makubwa mlioifanyia familia hii zaidi ya kusema asante na Mwenyezi Mungu mwingi wa rehema awalipe maradufu ya haya yote mliofanya.

No comments: