Monday, August 17, 2015

TANZANIA DMV WATOKA SARE 2-2 NA ZAMBIA

 Kocha mchezaji wa timu ya Tanzania DMV Dedi Luba akifuatilia mchezo kati ya Tanzania DMV walipocheza na Zambia siku ya Jumapili Aug 16, 2015 Silver Spring, Maryland na timu kufungana bao 2-2. Hii mechi ilikua ya marudiano katika mechi ya kwanza iliyochezewa Meadowbrook Park, Tanzania DMV waliishinda Zambia kwa bao 6-3. Katika mechi ya jana timu ya Zambia walikua wakiongoza kwa goli 1 mpaka mapumziko na waliongeza goli la 2 katika dakika ya 52 ya mchezo. Baada ya magoli hayo kuliizindua timu ya Tanzania DMV na kuweza kusawazisha magoli yote ndani ya dakika 15 za mwisho. Mpaka dakika 90 Tanzania DMV 2 Zambia 2.
 Kocha mchezaji Dedi Luba akitoa maelekezo kwa wachezaji wake kabla ya mchezo.
 Wachezaji wa Tanzania DMV wakimsikiliza kocha mchezaji Dedi Luba.

 Wachezaji wakiwa makini wakifuatilia maelekezo ya kocha wao Dedi Luba.

No comments: