ANGALIA LIVE NEWS

Sunday, August 2, 2015

TPA YASISITIZA MATUMIZI YA MFUMO WA KIILETRONIKI KWA WADAU WAKE


 Baadhi ya wadau wa bandari ya Dar es Salaam wakiwa katika kikao cha pamoja na viongozi wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari (TPA) kujadili maswala mbalimbali yanayolenga kuboresha huduma za bandari hapa nchini mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam.
 Kaimu Meneja Bandari ya Dar es Salaam (kushoto), Bw.Hebel Mhanga akifafanua jambo wakati wa kikao kati ya Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari (TPA) na wadau wa mamlaka hiyo mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam.  Kulia ni mkuu wa Usafiri na Miundombinu, Ofisi ya Rais, Matokeo Makubwa Sasa (BRN), Bw. Joy Mwalugaja.
Mkuu wa Usafiri na Miundombinu, Ofisi ya Rais, Matokeo Makubwa Sasa (BRN), Bw. Joy  Mwalugaja akiongea katika kikao hicho

Watumiaji wa Bandari ya Dar es Salaam wametakiwa kuongeza kasi ya utumiaji wa mifumo wa kiiletroniki kulipia huduma zinazotolewa na mamlaka hiyo ili kuongeza ufanisi wa kazi na kuondoa usheleweshaji wa uondoaji wa mizigo. Kaimu Meneja Bandari ya Dar es Salaam, Bw. Hebel Mhanga amesema matumizi sahihi ya njia za kielektroniki yatasaidia kwa kiwango kikubwa kuongeza ufanisi wa kazi katika bandari hiyo. 
 Akiongeana na waandishi wa habari baada mkutano kati ya Mamlaka ya Usimamizi wa bandari (TPA) na wadau wake jijini hapa mwishoni mwa wiki, Bw. Mhanga alisema wakati sasa umefika kwa wadau wa bandari kuzoea matumizi ya kielektroniki hasa katika malipo. 
 “Hapo ndipo tulipofika, dunia iko hapo...lazima tuendane na mabadiliko haya na kuleta tija katika kazi zetu wote,” alisema. 
 Akisisitiza matumizi ya kielektroniki alisema mbali ya kuleta ufanisi, kazi zinafanyikakwa uwazi zaidi na kuziba mianya ya ubadhirifu. 
 “Kwa sasa wateja wetu wanaweza kufanya malipo kupitia taratibu zilizoelezwa kwenye tovuti ya TPA na pia wanaweza kulipia kwa njia ya mitandao ya simu,” alisema. 
 Alifafanua kuwa kwa sasa hakuna sababu ya mteja kwenda bandarini kufanya malipo, bali mifumo hiyo inawezesha kulipia mahali mteja alipo na kwenda moja kwa moja eneo la kutolewa mzigo. Akizungumzia hatua nyingine za kuboresha utendaji kazi bandarini hapo alisema swala la kufanya kazi masaa 24 linazidi kuimarika. 
 “Kulikuwa na tatizo kwa baadhi ya benki lakini sasa wapo tayari kufanya kazi kwa muda huo,” aliongeza kusema. 
 Akitoamfano alisema benki ya NMB wapo tayari kufanya kazi kwa masaa hayo na kuwa benki nyingine wameongeza muda wa kazi hadi saa mbili usiku na hata kuongeza muda zaidi kulingana na mahitaji ya wateja. 
 Kwa upande wake, meneja wa forodha bandarini hapo, Bw. Wolfgang Salia alisema upo umuhimu wa haraka wakuwa na miundombinu bora ya barabara na reli ili kuimarisha zaidi huduma. 
 Mkurugenzi wa huduma za meli na bandari wa taasisi ya Intergovernmental Standing Committee on Shipping (ISCOS), Bw. Clement William alisema ufanisi pekee ndilo jambo litakaloifanya bandari ya Dar es Salaam kuvutia wateja. Bandari ipo katika mkakati mkubwa wa kupanua huduma na kuleta ufanisi na mikutano hiyo ya wadau imekuwa nimoja ya njia za kufanikisha azma hiyo.

No comments: