Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Bw.Paul Makonda akifafanua jambo alipokuwa akizindua Programu ya Kukuza na kuendeleza Ujasiriamali kwa vijana wa mkoa wa Dar es Salaam iitwayo Kijana Jiajiri mwishoni mwa wiki. Kushoto ni Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC), Bi. Beng’i Issa na Meneja wa Maswala ya Nje wa Tanzania LNG Plant Project, Bi. Patricia Mhondo ambao ndio wafadhili wa programu hiyo. Mradi huo unatekelezwa na Taasisi ya Kuendeleza Ujasiriamali na Ushindani Tanzania (TECC) kwa kushirikiana na Taasisi ya kuendeleza Vijana ki-biashara ya Uingereza (YBI) na NEEC.
Baadhi ya vijana wakimsikiliza mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Bw.Paul Makonda (hayupo pichani) wakati wa uzinduzi wa Programu ya Kukuza na kuendeleza Ujasiriamali kwa vijana wa mkoa wa Dar es Salaam iitwayo Kijana Jiajiri mwishoni mwa wiki. Mradi huo unatekelezwa na Taasisi ya Kuendeleza Ujasiriamali na Ushindani Tanzania (TECC) kwa kushirikiana na Taasisi ya kuendeleza Vijana ki-biashara ya Uingereza (YBI) na NEEC.
Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC), Bi. Beng’i Issa (kushoto) akifafanua jambo wakati wa uzinduzi wa Programu ya Kukuza na kuendeleza Ujasiriamali kwa vijana wa mkoa wa Dar es Salaam iitwayo Kijana Jiajiri mwishoni mwa wiki. Katikati ni Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Bw.Paul Makonda na Meneja wa Maswala ya Nje wa Tanzania LNG Plant Project, Bi. Patricia Mhondo ambao ndio wafadhili wa programu hiyo. Mradi huo unatekelezwa na Taasisi ya Kuendeleza Ujasiriamali na Ushindani Tanzania (TECC) kwa kushirikiana na Taasisi ya kuendeleza Vijana ki-biashara ya Uingereza (YBI) na NEEC.
Vijana mkoani Dar es Salaam na nchini kwa ujumla wametakiwa kujiamini na kuwa wabunifu kwa kuanzisha miradi ya ujasiriamali na kutumia fursa zilizopo kupiga vita tatizo la ajira ili kukukuza vipato vyao na kuchangia ukuaji wa pato la taifa.
Akizindua Programu ya kukuza na kuendeleza ujasiriamali kwa vijana wa mkoa wa Dar es Salaam na viunga vyake ijulikanayo kama Kijana Jiajiri, mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Bw. Said Meck Sadiq amesema vijana hawana budi kuonyesha juhudi na hamu ya kufanikiwa katika nyanja tofauti.
Kijana Jiajiri ni program ya kukuza na kuendeleza ujasiriamali kwa vijana wa Tanzania wenye umri wa miaka 18-35.
Inatekelezwa na Taasisi ya Kuendeleza Ujasiriamali na Ushindani Tanzania (TECC) kwa kushirikiana na Taasisi ya kuendeleza Vijana ki-biashara ya Uingereza (YBI) na Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC).
“Msikubali kuona ndoto zenu zinatoweka…mpambane huku mkijituma na kutumia fursa zilizopo kukuza vipato vyenu,” alisema katika hotuba yake iliyosomwa na Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Bw. Paul Makonda mwishoni mwa juma.
Aliwataka vijana hao kujitambua na kuyafanyia kazi mafunzo watakayopata kupitia program hiyo.
Aliwasisitiza vijana kutokubali historia ya umasikini wa familia zao, bali wajitume na kufanya kazi kwa bidii ili kuondokana na hali hiyo.
Akifafanua kuhusu mafunzo hayo, Katibu Mtendaji wa NEEC, Bi. Beng’i Issa alisema mafunzo hayo ya wiki sita yanawalenga vijana wa mkoa wa Dar es Salaam na viunga vyake ili kuwaptia elimu ya ujasiriamali.
“Hii ni programu ya kitaifa na mafunzo haya ni ya bure,” alisema na kueleza kuwa inaanza na mikoa mitatu ya Lindi, Mtwara na Dar es Salaam na kuwa baada ya mwaka mmoja mpango huu utapanuka kufikia mikoa mingine.
Program hiyo inadhaminiwa kwa ushirikiano wa makampuni matano ya kimataifa yanayojishughulisha na mafuta na gesi asilia hapa nchini ambayo ni BG, Statoil, ExxonMobil, Ophir na Pavilion Energy.
No comments:
Post a Comment