ANGALIA LIVE NEWS

Friday, August 7, 2015

WASANII WA MUZIKI WA BONGO FLAVOUR WAIKACHA SEMINA MUHIMU YA TCRA

 Nick wa Pili na G-Nako walihudhuria semina hiyo
Rapper Nick wa Pili ambaye ni mmoja ya wasanii waliolikwa na mamlaka ya mawasiliano Tanzania TCRA kwenye semina inayohusu masuala ya uhalifu wa mtandaoni Alhamis hii, ameshangazwa na muitikio hafifu wa wasanii wenzake.
Viti vitupu!
Nick amesema kati ya wasanii 70 waliokuwa wamealikwa kwenye semina hiyo, ni chini ya wasanii watano waliohudhuria.

“Tupo katika seminar ya wasanii wa bongo fleva iliyoandaliwa na TCRA….imeuzuriwa na viongozi wa juu na mkurugenzi ndio ataifunga, vyombo vyote vya habari viko hapa, polisi na polisi jamii,” ameandika Nick kwenye Instagram.

“LAKINI KATI YA WASANII 70, TULIO ALIKWA NI WASANII WA 4 TUUU….tulio udhuria….mimi, @vanessamdee @gnakowarawara na dabo. Ukiachia mbali elimu tuliyopata hawa TCRA…ni mdau mkubwa sana wa tasnia ya mziki. Tuache harakati za kulalamika….tufanye harakati za vitendo na uwajibikaji. Ukitaka vitu laini…lazima upitie vigumu….jamaa wamejiandaa vikubwa sana..wasanii mitini.”
Katika post nyingine, Nick aliandika:
Usiweke taarifa zako nyingi binafsi mitandaoni, Kuweka picha ya uchi mtandaoni ni kuvunja sheria….sheria na maadili ya tz haya ruhusu kuvuwa nguo hadharani. Huna haki ya kumpiga mtu picha akiwa katika mambo yake binafsi na kuiweka mitandaoni, Unapopost taarifa za ajali kumbuka…kaka,dada, mama, watoto….wa wahusika wanaweza kuona je watazipokeaje ghafla hivyo, Wasichana ndio wahanga wakubwa kuzalilishwa mtandaoni, Epuka kupiga picha hosteli ukioga ama kuvaa nguo pamoja.

No comments: