MPENZI wa mwanamuziki wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ Zarinah Hassan ‘Zari’ amejifungua mtoto wa kike leo alfajiri saa 10: 40 jijini Dar es Salaam. Mtandao huu umeongea na Meneja wa kimataifa wa Diamond Platinumz, Salam Sharaf ambaye amethibitisha taarifa hizo na kusema Zari bado yupo hospitali mpaka sasa.
Kutokana na usumbufu aliodai unaweza kutokea, Salam hakuweka wazi hospitali aliyojifungulia Zari. “Ni kweli Zari kajifungua mtoto wa kike majira ya saa 10 alfajiri leo, lakini kutokana na usumbufu unaoweza kujitokeza kwa sasa siwatajii hospitali aliyojifungulia mpaka hapo baadaye” Alisema Salam. Mtandao huu unatoa pongezi wa Diamond pamoja na Zari kwa kupata mtoto wa kike.
GPL
2 comments:
HONGERA DIAMOND AND ZARI KWA KUPATA MTOTO!MUNGU AWE NANYI NA AWALINDE!MTOTO!"WELCOME TO THE WORLD"
Congratulation to you Zari for your new Baby Girl. You are blessed. You wanted a Girl and you got it. Hongera Mwana muziki Diamond hongera sana sana umejaliwa mtoto mwenzetu ulitaka mtoto na Mungu kakujalia.
Hongera sana. Sasa kazi kwako kumlea na kumfundisha akuwe vizuri. Mungu awajalieni Zaidi. Karibuni. Welcome to USA. Mimi ni mama VRose niko Pittsburgh, PA
Post a Comment