Katibu Mkuuwa Wizaraya Kazina Ajira Bw. Eric Shitindi akitoa hotuba ya utangulizi juu ya Sheria Na. 20 ya Mwaka 2008 pamoja na uanzishwaji wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF) kulia kwake ni Waziri wa Kazi na Ajira Mhe. Gaudentia Kabaka
Waziri wa Kazi na Ajira Mhe. Gaudentia Kabaka akitoa hotuba kwa Wajumbe wa Bodiya Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF) pamoja na wageni waalikwa kabla ya kuzindua Bodi hiyo Rasmi.
Mwenyekiti wa Bodi Bw. Emmanuel Humba akitoa neno fupi na kueleza namna Bodi ilivyojipanga kuhakikisha malengo na madhumuni makuu ya uanzishwaji wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi yanafikiwa ikiwa na kuwahakikishia Fidia Stahiki Wafanyakazi Wote.
Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Fidia Kwa Wafanyakazi Bw. Masha Mshomba akipokea vitendea kazi pamoja na Sheria ya Fidia kwa Wafanyakazi Na. 20 ya Mwaka 2008 kutoka kwa Waziri wa Kazi na Ajira Mhe. Gaudentia Kabaka
Mwenyelkiti wa Bodi ya Wadhamini Bw. Emmanuel Humba akipokea chati cha usajili wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi Kutoka kwa Waziri wa Kazi na Ajira Mhe. Gaudentia Kabaka (Cheti cha Usajili kimetolewa na Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii Nchini SSRA)
Katibu Mkuu Wizara ya Kazi na Ajira Bw. Eric Shitindi wa pili kushoto, Mhe. Gaudentia Kabaka wakiwa katika picha ya pamoja na Wajumbe wa Bodi ya Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi.
Bodi ya Wadhamini ya Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi ilizinduliwa jana Septemba 4 katika ukumbi wa mikutano wa Wizara ya kazi na ajira jijini Dar. WCF ni Taasisi ya Serikali chini ya Wizara ya Kazina Ajira iliyoundwa kwa Mujibu wa Kifungu cha 5 cha Sheria ya Fidia kwa Wafanyakazi Na. 20 ya mwaka 2008 ili kushughulikia masuala ya fidia kwa Wafanyakazi waliopo katika Sekta ya Umma na Binafsi Tanzania Bara ambao wataumia, kuugua au kufariki dunia wa kiwa katika utekelezaji wa majukumu ya Mwajiri. MfukowaFidiakwaWafanyakazi (WCF) umeanzishwakwaMadhumunimakuuyafuatayo;
- Kutekeleza matakwa ya Sera ya Taifa ya Hifadhi ya Jamii ya mwaka 2003 katika kukabiliana na majanga mbalimbali yanayoikumba jamii ikiwamo ajali, magonjwa au vifo vinavyotokana na kazi;
- Kutekeleza matakwa ya Kifungu cha 5 cha Sheria ya Fidia kwa Wafanyakazi Na. 20 ya Mwaka 2008;
- Kulipa fidia stahiki pale mfanyakazi anapoumia, kuugua au kufariki kutokana na kazi;
- Kuwasaidia wafanyakazi watakaoumia au kuugua kutokana na kazi ili waweze kurudi kazini au kushiriki katika shughuli nyingine zitakazowapatia kipato (ukarabati na ushauri nasaha);
- Kuweka utaratibu utakaowezesha kuharakisha malipo yafidia kwa wafanyakazi au wategemezi wao;
- Kuweka utaratibu utakaowezesha Mfuko kupokea michango kutoka kwa waajiri na kufanya malipo;
- Kukidhi matakwa ya mikataba ya kimataifa kuhusu fidia kwa wafanyakazi; na
- Kukuza mbinu za kuzuia ajali, magonjwa au vifo katika maeneo ya kazi.
MajukumuyaMfukowaFidiakwaWafanyakaziyatakuwanipamojana;
- Kusajiliwaajirinawaajiriwa;
- kufanyatathminiyamazingirahatarishikatikasehemuzakazi;
- kukusanyamichangokutokakwawaajiri;
- kuwekezamichangoiliyokusanywa;
- kulipafidia pale mfanyakazianapoumia, kuugua au kufarikikutokananakaziwanazofanya;
- kutunzakumbukumbuzamatukioyaajali, magonjwanavifokutokananakazi.;
- kukuzambinuzakuzuiaajali, magonjwa au vifokutokananakazinakuelimishaummakuhusukazizaMfuko.
******
HOTUBA YA MHE. GAUDENTIA KABAKA (MB), WAZIRI WA KAZI NA AJIRA KWENYE UZINDUZI WA BODI YA WADHAMINI YA MFUKO WA FIDIA KWA WAFANYAKAZI KATIKA UKUMBI WA WIZARA YA KAZI NA AJIRA TAREHE 4 SEPTEMBA, 2015
Bw. Eric Shitindi, Katibu Mkuu, Wizara ya Kazi na Ajira;
Bw. Emmanuel Humba, Mwenyekiti, Bodi ya Wadhamini, Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi;
Wajumbe wa Bodi ya Wadhamini, Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi;
Wakuu wa Idara na Vitengo hapa Wizarani Wizarani;
Mkurugenzi Mkuu, Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Hifadhi ya Jamii (SSRA);
Bw. Masha Mshomba, Mkurugenzi Mkuu, Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF);
Mwakilishi, Shirika la Kazi Duniani (ILO);
Mwakilishi, Chama cha Waajiri Tanzania (ATE);
Mwakilishi, Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania (TUCTA);
Wageni waalikwa;
Mabibi na Mabwana;
Habari za asubuhi!
1. Awali ya yote ninapenda kumshukuru Mwenyezi Mungu, mwingi wa Rehema kwa kutujaalia uzima, nguvu na afya njema kwa kutuwezesha kukutana hapa leo katika siku hii muhimu.
Aidha,napenda nitumie fursa hii kutoa shukrani zangu za dhati kwa heshima kubwa mliyonipa ya kunialika kuwa Mgeni Rasmi katika hafla hii ya Uzinduzi wa Bodi ya Wadhamini ya Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi.
Pia, nitumie nafasi hii, kutoa pole kwako Mwenyekiti na kwa Wajumbe wote kwa kufiwa na mmoja wenu aliyekuwa Mjumbe wa Bodi ya Wadhamini ya ya Mfuko wa fidia kwa Wafanyakazi Marehemu Bw. Henry Nyamubi. Mungu amlaze mahala pema peponi Amina.
2. Ndugu Mwenyekiti na Wajumbe wa Bodi,
Napenda pia nitumie fursa hii kutoa pongezi zangu za dhati kwako wewe Mwenyekiti pamoja na wajumbe wote wa Bodi ya Wadhanini ya Mfuko wa Fidia kwa kuteuliwa kwenu kuwa wasimamizi wa shughuli za Mfuko huu. Ninazo taarifa kwamba, pamoja na Uzinduzi kutokufanyika kwa wakati, lakini kwa kutambua umuhimu, wa majukumu ya Bodi hii, tayari mlikwishaanza utekelezaji wa majukumu yenu. Ninawapongeza sana!
3. Ndugu Mwenyekiti na Wajumbe wa Bodi,
Sheria ya Fidia kwa Wafanyakazi Na. 20 ya Mwaka 2008, imetungwa kutokana na sababu mbalimbali, lakini kubwa ni kupitwa na wakati kwa Sheria ya Fidia kwa Wafanyakazi Sura 263 iliyotungwa toka Mwaka 1949 na kufanyiwa marekebisho mengi hivyo kuleta ugumu katika utekelezaji. Aidha, mafao yanayotolewa chini ya Sheria hii ya zamani ni machache na viwango vya malipo ya Fidia ni vidogo sana na hivyo kutokukidhi mahitaji ya sasa ya wafanyakazi pindi wanapoumia, kuugua ama kufariki kutokana na kazi wanazozifanya.
4. Ndugu Mwenyekiti na Wajumbe wa Bodi,
Kuundwa kwa Mfuko wa Fidia ni hatua muhimu sana kwa nchi yetu katika kupanua wigo wa Hifadhi ya Jamii nchini. Ujio wa Sheria Mpya ya Fidia kwa Wafanyakazi Na. 20 ya Mwaka 2008 ni mkombozi si kwa wafanyakazi pekee, bali hata kwa waajiri na Wananchi kwa ujumla. Hii ni kutokana na sababu kwamba, kupitia Sheria Mpya ya Fidia kwa Wafanyakazi, idadi ya mafao imeongezeka, viwango vya malipo Fidia kwa wafanyakazi na wategemezi wao vitaboreshwa, na hata utaratibu wa kushughulikia madai ya Fidia utaboreshwa. Tunatarajia kwamba hata mchakato wa kufuatilia na kulipa fidia utakuwa rahisi na wa muda mfupi zaidi kuliko ilivyo sasa.
5. Ndugu Mwenyekiti na Wajumbe wa Bodi,
Kazi kubwa niliyopewa kwa siku ya leo ni kuzindua Bodi ya Wadhamini ya Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi, lakini naomba nitumie fursa hii kueleza yafuatayo;
Bodi ya Wadhamini ya Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi imeundwa kwa mujibu wa matakwa ya kifungu cha 12 cha Sheria ya Fidia kwa Wafanyakazi, Na. 20 ya Mwaka 2008, na inajumuisha wajumbe kutoka
Serikalini, Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Vyama vya Wafanyakazi, Vyama vya Waajiri, OSHA, Benki Kuu, Taasisi za Elimu ya Juu, pamoja na wawakilishi kutoka kwa watu wenye ulemavu unaotokana na ajali ama magonjwa yanayotokana na kazi.
6. Ndugu Mwenyekiti na Wajumbe wa Bodi,
Katibu Mkuu ameelezea kwa kifupi madhumuni ya kuanzisha Mfuko wa Fidia pamoja na majukumu ya Mfuko. Mimi najielekeza kwenye majukumu ya Bodi ya Wadhamini. Majukumu ya Bodi ya Wadhamini ya Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi yameainishwa bayana katika kifungu cha 13 cha Sheria ya Fidia kwa Wafanyakazi, Na. 20 ya Mwaka 2008. Majukumu hayo ni pamoja na:
(i) Kusimamia uendeshaji wa shughuli za Mfuko;
(ii) Kutengeneza, kutekeleza na kupitia Sera zinazohusiana na Fidia kwa wafanyakazi kulingana na matakwa ya Sheria;
(iii) Kumshauri Mhe. Waziri wa Kazi kuhusu maswala yote yanayohusu Fidia kwa wafanyakazi, marekebisho ya sheria ya fidia kwa wafanyakazi , kanuni ama sheria nyingine zinazohusiana na Sheria hii;
(iv) Kukuza mbinu za kuzuia ajali na magonjwa katika sehemu za kazi kwa kushirikiana na Mamlaka ya Afya na Usalama mahala pa kazi (OSHA);
(v) Kutoa elimu juu ya haki na wajibu wa mwajiri, mfanyakazi na wategemezi wao.
7. Ndugu Mwenyekiti na Wajumbe wa Bodi,
Majukumu haya ni makubwa na muhimu sana kwa ustawi wa Mfuko. Hivyo nina matumaini makubwa kwamba, mtatekeleza majukumu hayo na mengine ambayo sikuyataja lakini yameelezwa katika Sheria husika ili kuhakikisha kwamba, Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi unakidhi matarajio ya wadau na kuleta tija na mahusiano mazuri sehemu za kazi. Hamkuchaguliwa kuwa Wajumbe kwa bahati mbaya isipokuwa
tulizingatia sana sifa mlizonazo pamoja na uzoefu wenu. Hivyo, tunaimani na nyinyi kwamba mtatumia weredi wenu kwa uadilifu katika kutekeleza majukumu yenu.
8. Ndugu Mwenyekiti na Wajumbe wa Bodi,
Taasisi mnayosimamia ni Sehemu ya Wizara ya Kazi na Ajira. Hivyo nitumie nafasi hii kuwakaribisha sana kwenye familia ya Taasisi zilizo chini ya Wizara ya Kazi na Ajira. Taasisi nyingine ambazo ziko chini ya Wizara ni pamoja na Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Hifadhi ya Jamii (SSRA), Shirika la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Shirika la Tija la Taifa (NIP), Wakala wa Afya na Usalama Mahali pa Kazi (OSHA), Wakala wa Huduma za Ajira Tanzania (TaESA) na Tume ya Usuluhishi na Uamuzi (CMA), Shirika la Hifadhi ya Jamii (NSSF).
Ni matarajio yangu mtatekeleza majukumu yetu kwa Ushirikiano wa karibu na Wizara pamoja na Taasisi nyingine kwa kuzingatia Sera, Sheria, Kanuni na mikakati ya Wizara.
9. Ndugu Mwenyekiti na Wajumbe wa Bodi,
Nafahamu kwamba zipo changamoto nyingi ambazo mfuko utakabiliana nazo hasa katika siku hizi za mwanzoni. Changamoto hizo ni pamoja na uelewa mdogo wa jamii kuhusu Mfuko huu, zoezi la kuwasajili waajiri wote wa sekta ya Umma na binafsi Tanzania Bara na uendelevu wa mfuko. Serikali kwa kushirikiana na wadau tutaendelea kuzikabili changamoto hizo hatua kwa hatua ili kuhakikisha kwamba malengo yaliyokusudiwa yanafikiwa.
Kazi kubwa iliyo mbele yenu ni kuhakikisha elimu na uhamasishaji unafanyika ili kuwezesha wafanyakazi na Waajiri wengi wanashiriki na kujiunga na mfuko huu.
10. Ndugu Mwenyekiti na Wajumbe wa Bodi,
Kwa kumalizia napenda kutoa shukrani zangu za dhati kwa maandalizi makubwa yaliyowezesha kufanikisha hafla hii, na ninawashukuru wote mlioshiriki kwa namna moja ama nyingine katika uzinduzi huu.
Baada ya kusema hayo machache, ninayo heshima kubwa kutamka kwamba, BODI YA WADHAMINI YA MFUKO WA FIDIA KWA WAFANYAKAZI imezinduliwa rasmi.
Asanteni kwa kunisikiliza
No comments:
Post a Comment