ANGALIA LIVE NEWS

Saturday, September 12, 2015

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA WIZARA YA UCHUKUZI MAMLAKA YA HALI YA HEWA TANZANIA

Simu: 255 22 2460735/2460706 FAKSI: 255 22 2460735/2460700 S.L.P. 3056 Barua pepe: met@meteo.go.tz DAR ES SALAAM Tovuti: www.meteo.go.tz
Unapojibu tafadhali nakili: Kumb. Na.: TMA/1622 12 Septemba, 2015.
Taarifa kwa umma: Upepo mkali unaoambatana na mawimbi makubwa unatarajiwa katika maeneo ya mwambao wote wa Pwani.
Taarifa Na. 201509-01 Muda wa Kutolewa Saa za Afrika Mashariki
Saa 6:00 Mchana
Daraja la Taarifa: Tahadhari Kuanzia: Tarehe

13 Septemba, 2015
Mpaka: Tarehe
15 Septemba, 2015
Aina ya Tukio Linalotarajiwa
Hali ya upepo mkali unaozidi kilomita 40 kwa saa (hadi kilomita 50 kwa saa katika baadhi ya nyakati) pamoja na mawimbi makubwa yanayozidi mita 2.0 (hadi mita 3.0 katika baadhi ya nyakati) inatarajiwa katika ukanda wote wa pwani.
Kiwango cha uhakika: Juu: (80%)
Maeneo yatakayoathirika
Mwambao wa bahari ya Hindi katika mikoa ya Tanga, Dar es Salaam, Pwani, Lindi na Mtwara pamoja na visiwa vya Unguja na Pemba.
Maelezo:
Hali hii inatokana na kuimarika kwa mgandamizo mkubwa wa hewa katika eneo la Kusini-magharibi mwa bahari ya Hindi na hivyo kusababisha upepo mkali wa Kusi katika pwani ya Afrika Mashariki.
Angalizo:
Mamlaka zinazohusika na maafa, watumiaji wa bahari na wakazi wa maeneo yaliyotajwa wanashauriwa kuchukua tahadhari.
Maelezo ya Ziada
Mamlaka ya Hali ya Hewa inaendelea kufuatilia hali hii na itatoa mrejeo pale itakapobidi.
Imetolewa na Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania.

No comments: