Bendi maarufu ya muziki wa dansi barani ulaya Ngoma Africa band aka FFU-ughaibuni ukipenda waiite viumbe wa ajabu Anunnaki Alien's yenye makao kule Ujerumani inatarajiwa kutingisha jukwaa katika maonyesho ya Vechelde Festival nchini Ujerumani Jumamosi 5. September 2015 saa 2:00 Usiku katika eneo la :Bürgerzentrum Vechelde liliopo mtaa Hildesheimer Straße 5 mjini Vechelde jirani mji wa Braunschweig,Ujerumani.Bendi hiyo maarufu Ngoma Africa yenye sifa za kuwatia kiwewe washabiki wa muzikikatika maonyesho ya kimataifa kwa kutumia mdundo wao "Bongo Dansi" made in Uswahilini ndio bendi pekee ya kiafrika barani ulaya iliyoweza kudumu kwa miaka 22 na kufanikiwa kukama soko la kutumbuiza katika maonyesho ya kimataifa. Kwa sasa bendi hiyo inatamba na CD yake mpya ya "LA MGAMBO" yenye nyimbo mbili za kumuaga rais Jakaya Kikwete na CD hiyo utunzi wake Kiongozi wa bendi Ebrahim makunja aka Kamanda Ras Makunja imeshatua nchini Tanzania tayari kwa kutingisha anga katika vituo vya redio mbali mbali.
wasikilize ffu-ughaibuni at www.reverbnation.com/ngomaafricaband
www.facebook.com/ngomaafricaband pia at www.instagram.com/ngomaafricaband
No comments:
Post a Comment