ANGALIA LIVE NEWS

Monday, September 7, 2015

Lowassa asema atapunguza mshahara wa Rais toka milioni 400 kwa mwezi hadi milioni mbili


Katika hotuba yake amesema haingii ikulu kutafuta fedha anaenda ikulu kwa kazi moja tu ya kuhakikisha wananchi wanakuwa na maendeleo . Amesema dhamira yake ni kuona taifa linasonga mbele kwa kasi ya ajabu.
Amesema atapunguza mshahara wa Rais ambao analipwa hivi sasa dola 192,000 sawa na milioni mia nne kwa mwezi hadi kufikia milioni mbili kwa mwezi amesema kuna faida gani ya mtu kupokea mshahara wote huo ili hali wananchi wako hawana maji , zahanati hakuna dawa, pembejeo za kilimo zipo juu, wakulima wanakopwa mazao yao.

Amesema haendi ikulu kutafuta ela amesema anaenda ikulu kwa kazi moja tu ya kuondoa umaskini nchini hiyo ndiyo dhamira yake.

Amewashangaa wanaosema anafuata fedha ikulu na kuwaambia kama mtu umeshindwa kutafuta fedha ujanani halafu utegemee upate fedha uzeeni hiyo ni ngumu kwa sababu uzeeni ni muda wa kusaidia jamii kwa kile ulichochuma ujanani.

Amesema wakati wa mabadiliko ni sasa, na mabadiliko hayo yatapatikana nje ya CCM kwani ipo haja ya kubadilisha mfumo hodhi wa chama tawala kama kweli tunataka kusonga mbele sisi kama taifa. Amesema yapo baadhi ya mambo CCM hawawezi kuyabadilisha kwa kuhofia watu watafumbuka macho hivyo itatishia uhai wao.
Source:Kengeteblog

7 comments:

Unknown said...

NAKUBALIANA NA MAWAZO YA MH LOWASA KWAMBA MABADDILIKO LAZIMA YAPATIKANE NJE YA CCM.KWAKUWA WAMESHINDWA KUBADILISHA MAISHA YA WANANCHI KWA ZAIDI YA MIAKA 50 JE LEO HII NDIYO WATABADILISHA?MIMI NIMEZALIWA TANZANIA NIKAKULIA TANZANIA MIAKA YANGU YOTE NILIYOKAA HAPO TANZANIA SIJAWAHI KULA MILO MIWILI KWA SIKU JE SERIKALI INAYOSHINDWA KUHUDUMIA RAIA WAKE LEO HII WANAWAOMBA TENA KURA NA KUWADANGAYA KWAMMBA WATABADILISHA MAISHA YAO SIYO KWELI.MIMI NILIKUWA NA UWEZO MZURI SANA WA KIMASOMO LAKINI NILIJARIBU KUOMBA MKOPO SIJAPATA HADI NILISHINDWA KUMALIZIA ELIAMU YANGU YA JUU HIVYO NINAJUWA KUNA WENGI AMBAO WAKO KAMA MIMI WANAOSHINDWA KUMALIZA MASOMO YA0 KWAKUWA HAWAKO NA WATU WATAKAO WASIMAMIA KWAKUPATA MIKOPO.HIVYO NINGEWASHAURI RAIA WOTE WA TANZANIA WAFANYE MABADILIKO MWEIZ WA KUMI ILI WAONE VIPI RAIS MWENGINE ATAKAVYOFANYA LAKINI WAKACHAGUA WALEWALE MAISHA YAO YATAKUWA YALEYALE.

Anonymous said...

Safari zake za kutubiwa German mara kwa mara ndiyo zina impact kwa ktk maendeleo ya Tanzania.

Anicetus said...

President Obama 2014 Tax report show net income of $477,383.00 dollars. The average monthly income was $39,752 or. Tz $ 83,420,000.00 per month.
How come Tanzania president rated the as one of the poorest countries in the world pay his president 4 times as much and the presindent of the richest country in the world.

If Lowassa wins, he will pay himself a salary of Tz$200,000,000 which is 2 times the salary of the president of United States.

Anonymous said...

This is too much beyond imagination or any expectation! 400 million a month na bado wanaiba hela za wananchi escrow na megineyo kweli wanastahili kuchomwa moto hadharani. plz post this and dont be bias kupendelea ccm

Anonymous said...

Kumbe sasa ninaelewa kwa nini IKULU walipata kigugumizi kutaja fedha za mshahara wa Kikwete. Tuangalie kwa hesabu kidogo tu. Mtoto mmoja kwa mwaka shule ya msingi ni dola 100 kwa mfano! Sasa mshahara wa kikwete utawepeleka watoto wangapi shule? 192,000 dola/mwezi x 12 = 2,304,000 / 100 = 23,400 watoto!! Je ikiwa mshahara wa waalimu ni dola mia kwa mwezi utawalipa waalimu wangapi? Ukipiga hesabu ndogo too...ni waalimu zaidi ya 15,000!! Eeh...karibu Tanzania Mpya, Karibu Ukawa. Karibu Lowassa. Ukiweza kukata TANESCO; Ukakata Mawaziri; Ukakata ushenzi wa kubadili mabalozi kila asubuhi na jioni! Ukikata kwenye kodi - TAYARI PESA YA KUPELEKA WATOTO MPAKA CHUO KIKUU ZIPO! UKIAKATA TRA; UKIKATA BANDARINI; UKIKATA TWIGA; UKIKATA MADINI TAYARI PESA YA HOSPITO NA MAJI TANZANIA NZIMA! EEEH, NCHI YENYE REHEMA KWA WATANZANIA WOTE INAKUJA SI NCHI YA WATU WATATU AU WANNE ETI KWA SABABU BABA ZAO WALIKUWA KWENYE SYSTEM! Thanks LOWASSA. UKAWA NA LOWASSA NI MPANGO WA MUNGU!

Anonymous said...

Grossly inaccurate statistics! Who told you the Tanzanian President's salary is $192,000 per month? It's not plausible, even without doing any research. In comparison, the U.S. President makes only $400,000 per year, approximately $33,333 per month!

Anonymous said...

Shame to African readers if a Tanzania president gets 400 million shillings amonth. kama kweli CCM ndio waliopanga huo mushahara wa raisi milioni mia nne kila mwezi,basi ndiyo maana wananchi wanataka mageuzi.Ndugu zangu hapo Nhakuna huruma hata kidogo.Dakitari na walimu waanapata ngapi?Sasa tunatamani mwalimu Nyerere angerudi asigekubali kuwa ni CCM aliyoanzisha. Tunaipenda CCM hile ya mwalimu iliyomjari kila mwana nchi.Ebu katika kampeni za sasa hivi wanbie wana nchi kama watakuelewa.Ndiyo maana kila kiongozi anataka fedha tu hana haja ya wananchi.Kama sio Ukawa kusema mushahara wa rais wananchi wasingejua.Mimi ni mkeleketwa wa CCM moyo wauha nikisikia hayo.Inavunja moyo tunakosa mwenzetu wakumuamini.