Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad akizungumza na Balozi wa Tanzania nchini Zimbabwe huku ofisni kwake Migombani mjini Zanzibar.
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad akisalimiana na Balozi wa Tanzania nchini Zimbabwe huku ofisni kwake Migombani mjini Zanzibar.(Picha na Salmin Said OMKR)
Na Khamis Haji OMKR.
Makamu wa kwanza wa Rais wa Zanzibar, Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad amesema wananchi wa Tanzania na Zimbabwe wanayo nafasi nzuri kukuza maendeleo yao iwapo fursa za kiuchumi na biashara zilizopo zitazidi kuibuliwa na kufanyiwa kazi.
Maalim Seif amesema hayo leo wakati alipokuwa na mazungumzo na Balozi wa Tanzania nchini Zimbabwe, Charles Makakala aliyefika ofisini kwake Migombani kwa ajili ya kujitambulisha baada ya kuteuliwa kushika wadhifa huo.
Makamu wa Kwanza wa Rais amesema mbali na nchi hizo kuwa na uhusiano wa kidugu, lakinia pia ni wanachama wa Umoja wa Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC), hivyo malengo yao ya kiuchumi na kibiashara yanafanana.
Amesema hivi sasa kuna Watanzania wengi wakiwemo kutoka Zanzibar wanaofanya biashara nchini Zimbabwe, kama ilivyo kwa wafanyabiashara wa Zimbabwe nchini, hivyo ni dhahiri mafanikio makubwa zaidi yatapatikana, iwapo mazingira ya kibiashara yataimarishwa zaidi.
Naye Balozi Makakala ameahidi kuwa atajitahidi kutekeleza diplomasia ya kiuchumi, na kuzidi kuibua fursa zote za kiuchumi na kibiashara kwa azma ya kuimarisha mazingira bora ya kufanya shughuli hizo kwa maslahi ya wananchi wa nchi mbili hizo.
Balozi Makakala ametuliwa kushika wadhifa huo, baada ya mtangulizi wake, Balozi Adadi Rajabu kumaliza muda wake na sasa ameingia katika harakati za kuwania nafasi ya Ubunge katika uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 25 mwaka huu.
No comments:
Post a Comment