ANGALIA LIVE NEWS

Sunday, September 13, 2015

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI


TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI  
Taarifa ya kuanguka Msikiti Makhah-Saudi Arabia, Watanzania Salama.
Kufuatia mvua  ilioambatana na upepo mkali na kusababisha kuanguka kwa mashine ya ujenzi wa upanuzi wa eneo la Tawaf ulipo msikiti wa Makkah, msikiti huo umeanguka na kusababisha vifo vya mahujaji.  
Kwa mujibu wa Televisheni ya Saudi Arabia, Saudi TV hadi sasa watu 107 wamefariki dunia na wengine takriban 200 wamejeruhiwa. 
Kufuatia ajali hiyo, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa kupitia Ofisi za Ubalozi Riyadh unathibitihsa kuwa Mahujaji wa Tanzania wameanza kuwasili Jeddah kuelekea Makkah leo tarehe 12 Septemba 2015 wakitokea Madina. Hadi sasa Wizara haijapokea taarifa ya Watanzania waliopoteza maisha wala kujeruhiwa kwenye ajali hiyo.
MWISHO.
Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali kwa Umma,
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa,
12 Septemba, 2015

1 comment:

Anonymous said...

Uandishi ni fani, kama zilivyo fani nyinginezo kama udaktari, uhandisi n.k
Nasikitishwa sana na kitengo cha wizara muhimu kama Mambo ya nje kinatoa tangazo ambalo kichwa cha habari ni potofu au kina vumisha badala ya kutoa taarifa.
Msikiti wa Makkah haukuanguka, kilicho anguka ni Crane ambayo iliangukia kwenye sehemu mojawapo ya msikiti na kuua na kujeruhi waumini walokuwa wakifanya ibada katika eneo hilo.
Kitengo kama cha mawasiliano cha wizara ni lazima kitakuwa na watu ambao wanaandika, kuyapitia maandishi na kisha kuyapitisha.
Kuandika kuwa msikiti wa Makka umeanguka ni uzushi na inaleta tafsiri tofauti kwa msomaji wa taarifa hiyo.
Msikiti wa Makka ni msikiti mkubwa kuliko yote duniani, ndani ya msikiti kuna kaaba ambapo modern geographical scientist wameprove kuwa ndio center of the world.
Eneo la msikiti wa Makka ni takriban Ekari 88, crane moja haiwezi kuangusha msikiti wa ukubwa wa eneo hilo. Kwa mfano wa Tanzania, eneo la uwanja wa Taifa (mpya) ni karibu sawa na msikiti wa Makka, sasa pangekuwa crane imeanguka uwanjani hapo na kuua na kuumiza watu, then iandikwe uwanja wa Taifa umeanguka is something that will be exaggerated for certain ill gotten reasons but will not be the facts.
Ni issue sensitive na ningependa kuona hicho kitengo cha habari hapo wizarani kinasahihisha hiyo statement na kusema kilicho sahihi.
Kutofanya hivyo itakuwa ni kukusudia kuandika kilicho andikwa, lakini hadi sasa naweza kutoa nafasi ya shaka kuwa waloandika walipitiwa, but wafanye masahihisho.
Ahsante.