ANGALIA LIVE NEWS

Saturday, September 5, 2015

TUJIFUNZE NINI TOKA MAJIRANI ZETU KUHUSU FAIDA YA KUTANGAZA NCHI?

Habari na picha za Freddy Macha Fahari ya Kenya. Maonesho ya uzuri na urembo Tamasha la “Kenya in the Park”- Jumamosi iliyopita, tarehe 29 Agosti 2015, lilifana sana. Tamasha kama hili limewahi pia kufanywa mara nyingi na Ghana. Faida yake nini? 1. Kutangaza nchi. Kuendeleza wajasiriamali, elimu, wasanii, nk 2. Kukutanisha wananchi. Kuwaunganisha. Urafiki. Uzalendo. Kujuana. NETWORKING, kwa Kimombo. 3. Wageni huwajua na kutaka kuwatembelea. Utalii, kuwekeza na kuunga mkono miradi mbalimbali. Tamasha hili lilikuwa na watu wa nchi mbalimbali waliokiri kuifagilia sana Kenya! Ulikuwa pia wakati Kenya ilipoongoza kwa medali za Riadha, mjini Beijing. 4. Sanaa na Michezo. Vigezo vinavyokuuza uchumi. Tutafakari namna mataifa kama Jamaica na Brazil yanavyofahamika kutokana na fani hizi

5. Kurahisisha mawasiliano ili panapotokea janga au zuri iwe rahisi kueleweshana. Starehe, vifo, kampeni za Ebola, Malaria, UKIMWI nk 6. Paki zina urahisi zaidi kuliko maholi ya kifahari yenye gharama kubwa. Yote yanayofanyika katika kumbi za densi yanawezekana viwanja safi vya Uingereza : densi, vyakula, vinywaji, kujamiiana, nk. Mkenya na mkewe wakifurahia siku hiyo uwanja wa West Ham, London. Mohammed Juma wa Mombasa akishughulika na nyama choma, ndizi mzuzu za kuoka nk. Mtayarishaji wa maonesho, msanii na mwanahabari, Lydia Olet, akiwa na wacheza sarakasi toka Ghana Baadhi ya mambo yaliyofanywa na Wakenya yalikuwa 1. Michezo kama ngumi 2. Starehe za watoto 3. Warsha za Ngoma asilia za Kiafrika na Kenya 4. Wasanii toka nchi nyingine za Afrika 5. Maelezo ya Wakenya wanaofanya ya maana Uingereza, nini kiini cha Wimbo wao wa Taifa, nk 6. Hotuba fupi ya Balozi Mhe. Lazarus Amayo 7. Biashara za mali asilia toka Kenya kama kanga, vitenge, fulana nk 8. Maonesho ya uzuri, mavazi, sanaa na urembo 9. Maonesho ya muziki. Wanamuziki toka Kenya, Uingereza, Congo, Uganda, Tanzania, Sierra Leone, Ghana, nk 10. Usingaji na masuala ya Afya 11. Vyakula mbalimbali vya Kenya : Ugali, Nyama Choma, Sukumawiki, Chapati, Makongoro, Ubwabwa nk 12. Vyakula vya nchi nyingine Afrika Mashariki mathalan, Ethiopia. Mkenya akichangamkia hali kwa kinywaji Wana Afrika Mashariki. Mwanahabari mkongwe , Deo Kamugisha (wa kwanza kulia) akiwa na Mtanzania Abdallah (kwanza kushoto) na rafiki toka Uganda Mkenya Lydia Makale akiwa na mwanarapu chipukizi wa London, Septimus Prime Mwana Kitoto na Wapambe husika wa tukio...

Baadhi ya wasanii nyuma ya jukwaa kabla ya kufanya maonesho yao
Mamii wa Kenya akifurahia msosi. Ubwabwa. Mzawa wa Mombasa, Billy Mwangura, mpiga besi wa bendi la Afrika Jambo
Mpiga gitaa mashuhuri na kiongozi wa bendi ya Afrika Jambo, Kawele Mutimanwa akiwa na wapambe toka Uganda.
Waghana wakisheherekea siku yao (kama hii) mwaka jana. Picha ihsani ya Akwaaba UK. http://akwaabauk.com/wp-content/uploads/2014/08/IMG_0469.jpg
Mwana Kitoto na msanii wa ACD Arts, Steven Kasamba toka Uganda. Picha na J J Adamson wa Africans in London TV. Habari zaidi tembelea: www.kenyainthepark.com

No comments: