ANGALIA LIVE NEWS

Sunday, September 6, 2015

VIONGOZI WA TAASISI ZA VIJANA WAKUTANA KUJADILI MTAALA WA KUFUNDISHIA ‘UJASIRIAMALI USIOATHIRI MAZINGIRA’

Viongozi wa taasisi za vijana kutoka kwenye nchini sita wamekutana mjini Bagamoyo kujadili na kuandaa mtaala utakaotumika kuwafundisha vijana namna ya kufanya ujasiliamali usioathiri mazingira “Green Entrepreneurship”.
Mkutano huo ambao ulitanguliwa na ziara ya mafunzo kwenye Shirika la Maendeleo ya Nishati  Mbadala (TaTEDO), umewashirikisha viongozi wa taasisi za vijana kutoka Slovenia, Italia, Nepal, Ureno, Argentina na wenyeji Tanzania walipata fursa ya kujifunza namna ya uzalishaji wa nishati mbadala isiyoathiri mazingira.
Shukuru Meena, Mratibu wa miradi ya nishati kwenye Shirika la Maendeleo ya Nishati  Mbadala (TaTEDO).
 Picha ya pamoja wakati viongozi hao walipotembelea TaTEDO.
Chris Ndallo (kushoto), Mtendaji Mkuu wa shirika la Maendeleo ya Vijana TYCEN akijadiliana jambo na baadhi ya watumishi wa TaTEDO.
Viongozi wa taasisi za vijana, wakitazama baadhi ya miradi inayoendeshwa na TaTEDO wakati walipotembelea ofisi za shirika hilo.

No comments: