Friday, October 30, 2015

Mbowe na mustakabali wa CHADEMA


Kwa kweli nimesikitishwa sana namna chama mahiri cha upinzani kama CDM kudhalilika kiasi hiki katika uchaguzi huu mkuu. Niliipenda CDM-Asilia lakini ilipoingiliwa na wana CDM-Maslahi niliamua kuitosa na kumpigia debe Magufuli.
Uchaguzi umekwisha na tunae Raisi. 
Je Tunao Upinzani Mahiri Tena?
Kwa kweli CDM imeathirika sana na inaweza kumeguka vipande vipande. Kwa sasa naona ACT-Wazalendo wanaweza kupata wafuasi wengi sana na kuwa chama kikuu cha upinzani ifikapo 2020. Sidhani kama tuna upinzani mahiri tena kwa sasa.

CDM Wafanye Nini Sasa:
Cha kwanza ni kumng'oa haraka sana yule rubani aliebadilisha gia angani na kukiangamiza CHOMBO.
YES, lazima mheshimiwa Mbowe awajibike haraka sana kama wana CDM watakuwa na imani tena na chama chao, la sivyo itakuwa ni mafuriko kuelekea ACT, au CCM. Leadership ethics zinamshinikiza Mbowe aachie kiti.
Utabiri wangu uchwara ni kuwa sidhani CDM inaweza kuji-rehabilitate tena katika miaka mitano ijayo. Pengine ni mpaka 2025 ndio wanaweza kuwa na nafasi ya kuwania uraisi ikiwa tu mabadiliko katika ngazi za juu yawe yalishafanyika jana.
Katika mabadiliko haya ya ngazi za juu ni muhimu CDM wasiwape waTanzania hisia ya kuwa hiki ni chama cha watu wa kanda ya kaskazini - itawagharimu sana.
Tanzania haiwezi kusonga mbele kama chama tawala hakiwezi kuogopa kuwa kuna upinzani mahiri. Kwa anguko hili la CDM na UKAWA, Tanzania hakuna upinzani tena, trust me.

Sheikh Mbowe mdogo wangu, kiongozi wangu, jipime halafu ukinusuru chama. Bado muda upo lakini hii window of opportunity ni fupi sana.
source - jamii forums

8 comments:

  1. WEWE NI KICHAA WA CCM?AMA KWELI DUNIA HII IMEJAA WAOKOTA MAKOPO WALIOVAA SUTI.YAANI NIMEKEREKWA KWELI KWELI NA ANONYMOUS 8.04 PM ANAPOHOJI "JEE TUNAO UPINZANI MAHILI TENA"? LA KWANZA UNAPASWA KUELEWA KUWA MSHINDI HALALI WA KITI CHA URAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA NI MHESHIMIWA EDWARD NGOYAI LOWASSA WA CHADEMA-UKAWA KWA KUPATA KURA [ZA UHALISI] MILLION 10,268,795 SAWA NA ASILIMIA 62 YA KURA ZOTE ZILIZOPIGWA.SISI WANANCHI TUNAYATAMBUA MATOKEO HAYO NA SI HAYO YA WIZI MTUPU YALIYOTANGAZWA NA TUME YA TAIFA YA UCHAGUZI.SASA WEWE UNAULIZA UPINZANI WAULIZE CCM KWA KUWA WAO SASA NDIO WAPINZANI WAPYA.NAKWAMBIA HIVI KUANZIA LEO KWA SIKU 1865 YAANI MIAKA MITANO IJAYO TUTAENDELEA KUMTAMBUA MHESHIMIWA LOWASSA KUWA NDIYE RAIS HALALI KWA MUJIBU WA KURA ZA WANANCHI WA TANZANIA.TUTAMWITA MHESHIMIWA RAIS,TUTAMUENZI,NA LA MSINGI ZAIDI TUTAENDELEA KUKIJENGA CHAMA UKAWA-CHADEMA KWA NGUVU ZETU ZOTE HUKU WABUNGE WETU WAKITEKELEZA KAZI ZA WANACHI KUPITIA BUNGE LETU NA MADIWANI WETU KWA MAMIA WAKIENDESHA MAJIJI,MANISSPAA NA HALMASHAURI NCHINI KOTE TULIKOWAVUA CCM UONGOZI.HABARI NDIYO HIYO,WAPELEKEE WALIOKUTUMA.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Are you in a deep denial? You must have lost your mind. Please surrender yourself to a competent psychiatrist as soon as possible! You cannot force victory for your corrupt candidate. The presidential election has never been freer, more fair and more transparent in our country history than it was this time. The election could be repeated ten times and your corrupt UKAWA candidate would consistently lose to Tingatinga. Tanzanians are not that stupid to mortgage their country to a group of thugs.

      Remember, a hyena is just a hyena, whether in Serengeti National Park or in Mikumi National Park. A hyena doesn't become a deer by simply moving from one park to another. ENL was a hyena within CCM and so will he continue to be within his newfound home, UKAWA. It's that simple.

      By the way, based only on my analysis of your writing style, I am pretty sure I have run into your posts numerous times before and have always raised my concern about your reasoning ability. You're either a brainwashed SOB or just a mentally-challenged human being from birth!

      Delete
  2. Najibu swali "jee tunao upinzani mahiri tena?" toka kwa anonymous 8.04 pm [nakuhisi wewe ni msaliti dr.slaa]Kwa mara ya kwanza nchini tanzania bunge la jamhuri ya muungano wa tanzania litakuwa na wabunge wa upinzani wengi mno, 106,ongezeko la wabunge 22,narudia ongezeko la wabunge wa upinzani 22 toka wabunge wa upinzani 84 bunge lililomaliza muda wake.sasa wewe pimbi wa ccm hili ongezeko la wabunge 22 unalionaje? hii ni excellent significant improvement ya 25%.wewe mbung'o hulioni hilo,ivi kweli wewe umetengemaa au ni ROBBOT WA CCM?sasa ngoja uusikilize huo muziki mnene utakaokuwa ukitoka bungeni.ccm mtakua matumbo-joto kwa miaka yenu yote hiyo mitano.msukosuko baada ya msukosuko,ni adhabu.hapa kubenea hapa mwita marwa,hapa esther bulaya,kule sugu,kule profesa j,hapa mbatia,kule mbowe, wanakuja,wanakuja niseme nini.

    ReplyDelete
  3. Usinichekeshe wewe anony. wa 1:22 AM. Jamani, what lessons has ukawa/Chadema learned? Unasema mnataka kuwa Chama cha Taifa/nchi nzima? You need to reform the party kama anony. #1 alivyosema na achana na hii childish mentality. You have to market yourself thoroughly well beyond kilimanjaro and Arusha, otherwise Chadema itakuwa inaokota kura ndogo ndogo hapa na pale which won't be enough to make a deep dent on CCM monopoly of Tanzania's politics. Huo Ukaskazini, Uchaga, Uarusha wenu don't resonate well in Mwanza, Dodoma, Ruvuma, etc..The "SISI wa Kaskazini" crap should be the thing of the past, because Tanzanians prefer a party which can Unite 120 tribes..i.e. Umoja kwa Watanzania Wote. This non-sense that Lowasa is your president is depressing, and very myopic. You are a victim of the "UKASKAZINI" disease, and so is Mbowe, Sumaye, and the likes. Lowasa, was rejected by many Tanzanians at the ballot-box, as witnessed by International observers. Of course, it is your prerogative to worship him as your president as long as you wish, but to what good? Is this Fantasy versus Realty? Instead of whining and CCM bashing, I beg you to be an agent of change and perhaps, 10-15 years from now, a post-Lowasa/Mbowe Chadema becomes a uniting National and Not Regional Political Party anymore!

    ReplyDelete
    Replies
    1. This is a very fair response to a brainwashed and helpless kid! I repeat, a "kid"! It doesn't matter how old (s)he may be, because (s)he reasons childishly, to say the least!

      Delete
    2. Naunga mkono hoja You nailed it down very well. .

      Delete
  4. sema utakalolitaka na utakaloliweza kulisema uhuru unao na ccm imekunufaisha sana,haukua na cv za kuletwa marekani,ulibebwa na kikwete kama furushi uje marekani "kula bata" ati kwa kua baba yako alikua rafiki kipenzi wa mzee mrisho.magufuli atakuumbua,utarudi tanzania .na kwa kua akili huna utarudia ile kazi yako ya zamani kushona viatu pale chalinze njia panda. sikiliza ccm ni wezi wakubwa wa kura,ni majambazi wa siasa,ni hatari kwa amani na ustawi wa tanzania.ipo siku wataachia tuu,mapambano yanaendelea.

    ReplyDelete
  5. Hivi ninyi waporipori wote hamna
    Lakufanya zaidi ya kubishana Magufuli, Lowasa, Kikwete, Dr Slaa wote ni wale wale ukombozi bado tutaendelea kukaa gizani na kuoga na mabeseni na ndoo mpaka mkombozi ambaye hatujui yuko wapi kwa sasa atapojitokeza ( labda mwanao ambae ni 1 year old atakapokuwa kwa sababu I'm sure hao hawatakuwa na mawazo duni kama Watanzania wa sasa)

    ReplyDelete

bila kutumia lugha ya matusi na kumharibia mtu siku
yake