Advertisements

Saturday, October 31, 2015

MFANYABIASHARA DAVIS MOSHA ATANGAZA KUTOGOMBEA UBUNGE JIMBO LA MOSHI MJINI

Aliyekuwa mgombea Ubunge jimbo la Moshi mjini,mfanyabiashara Davis Mosha akizungumza katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika viwanja vya Penfold kwa lengo la kuwashukuru wana CCM waliompigia kura.
Baadhi ya wana CCM waliohudhuria mkutano huo.
Mfanyabiashara Davis Mosha akitangaza uamuzi wake wa kutojihusisha tena na siasa,uamuzi uliosababisha wanaccm kushindwa kujizuia na kuanza kuangua vilio.
Baadhi ya wana CCM wakilia kwa uchungu mara baada ya Davis Mosha kutangaza kutogombea tena Ubunge .
Katibu Mwenezi wa CCM mkoa wa Kilimanjaro,Michael Mwita alilazimika kwenda kumuomba kubadili uamuzi wake huo.
Vilio havikuwa kwa wanawake peke yao hata wanaume walishindwa kuvumilia.
Wengine walitishia kujinyonga mbele yake.
Uamuzi wa Davis Mosha kuamua kutogombea tena Ubunge unatokana na kile alichodai kuwa baadhi ya viongozi wa CCM kushiriki kumuhujumu katika harakati za kuwania ubunge.
Wengine sura zao zilibadilika zikawa tofauti na zile tulizozizoea.
Mwenyekiti wa CCM manispaa ya Moshi,Elzabeth Minde aliingilia kati kujaribu kuomba Mosha kubadili uamuzi wake huo bila ya mafanikio.
Wanaccm wengine walilazimika kupanda jukwaani bado walizuiliwa.
Wengine walizimia  na kupatiwa msaada wa huduma ya kwanza.
Mosha aliondolewa uwanjani hapo chini ya ulinzi mkali wa Polisi kutokana na wanachi walioonekana kutofurahishwa na uamuzi wake huo.
Msafara wake ulisindikizwa na askari Polisi.

Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini.

3 comments:

Anonymous said...

POLE BWANA MOSHA,DUNIA NDIVYO ILIVYO.WALE WALAFI WALIOMO NDANI YA CCM WAKIONGOZWA NA BONGE WILLIAM MALECELA[CAMPAIGN SUPERVISOR WAKO] WALIKUPELEKESHA NA KUKUFANYA UAMINI NA KUJIAMINI KUWA UNAWEZA KULICHUKUA JIMBO LA MOSHI MJINI.LAKINI ULITAKIWA UTUMIE TUU AKILI ZAKO,TENA,KIDOGO SANA-KIDUCHU- NA SI KUPELEKESHWA.UMEHONGA SANA, UMETEKETEZA MABILIONI, UMEWATUMIA VIJANA WA KULIPWA NA WEWE KWA MAMIA,UMEONGOZA FUJO NYINGI SANA,RAIA KUPOPOLEWA NA MAWE NK.HUKUJUA WILLIE MALECELA "ZE MUTUZ" KAMA ALIVYO NI TAPELI,MUHUNI,MPENDA VIMWANA,ANA AKILI MBAYA, TENA MBAYA SANA NA KWA KWELI AMEKUUMIZA SANA MOSHA,UMEUMIA.UNAKUMBUKA YEYE[WILLEY] ANAKUITA SUPER BILLIONEA,SUPER MOGUL DAVIS MOSHA.UNA HELA GANI WEWE DAVIS KUWANUNUA WAPIGA KURA WA MOSHI MJINI?WAMEKUKAANGA WAPAMBE NA INAELEKEA UPO UKINGONI MWA UMAARUFU WA KUWA NACHO KWA SABABU WEWE NA WAPAMBE WAKO MMEFANYA FUJO, KUFURU NA UMAFIA VINAVYOKATAZWA NA MWENYEZI MUNGU.SASA UNAAPA UNAACHA SIASA,HUTOGOMBEA TENA,POLE DAVIS.

Anonymous said...

achene ujinga hiyo sanaaa. sasa naye anakuwa kama ukawa kutengeneza habari

Anonymous said...

Hahaaa chezea chagazi wanakukunywa wanakutelekeza sidumu fikiraa sa papa
msasii Arawa na Uncle Mangi