Tuesday, October 6, 2015

Mwalimu Nyerere akizungumza kuhusu Upinzani kuchukua Nchi mwaka 1995

2 comments:

  1. Hotuba hii ya Mwalimu Nyerere ilitolewa miaka 20 iliyopita, na ushauri huo kwa vyama vya upinzani nadhani ulizingatiwa. Kwa hiyo sasa ni wakatai muafaka kwa upinzani kuongoza nchini hasa kwa vile miaka 20 baada ya hotuba hii na baada ya chama cha CCM kubakia madarakni wakati wote, wanainchi hawajaona mabadiliko katika hali ya maisha yao, wanaendelea kubakia fukara katika nchi iliyojaa neema za mali asili na wakati huo huo viongozi wa serikali na wanasiasa wengi wa CCM wakiendelea kujitajirisha kwa hali ya kukufuru. Bila shaka Mwalimu angelikuwa hai leo hii angekubaliana na Mzee Kingunge kwamba CCM imeishiwa pumzi na sasa ni wakati muafaka kwa CCM kukaa benchi iwaachie wengine nafasi ya kuongoza nchi. Licha ya kasoro ndogo ndogo, upinzani nchini Tanzania umekuwa na umefikia hatua ya kuweza kuongoza nchi.

    ReplyDelete
  2. Upinzani ulianza kuelekea kuwa na nafasi nzuri ya kushika nchi kama mbadala wa CCM kama ungeendelea na sera zake zilizofanya ukaanza kukomaa. Bahati mbaya na shauri ya tamaa ya fedha upinzani umepotoka baada ya kufuata mkondo ambao ndiyo ulikuwa inaupiga vita. Kwa kuruhusu mafisadi kujiunga na kujihifadhi ndani ya upinzani, hususan Chadema/Ukawa jambo hili limeweka dosari kubwa sana katika harakati ya vyama hivi. Kwa hali hii CCM ambayo ilikuwa inapigiwa kelele kwa kuficha mafisadi sasa inasimama kidedea baada ya kuwatua watuhumiwa wa ufisadi. Ni kipindi kifupi tu kilichopita Chadema/ukawa walikuwa wanatembea kifua mbele kwa wananchi wakiongelea maswala ya ufisadi, lakini leo hata kwenye kampeni mgombea wao ameshindwa hata kulitamka neno fisadi kwani yeye ndiye aliye kuwa mtajwa mkuu katika uozo huu. Sasa leo Watanzania wataelewa vipi upinzani ukiwambiwa wanataka kuleta mabadiliko yenye lengo la kufuta ufisadi ikiwa mafisai wenyewe ndiyo wanahamia kwenye upinzani!
    Maneno ya Kingunge Ngombale Mwiru hayana uhusiano wowote na maoni ya Mwalimu. Ni kweli kabisa kuwa Mwalimu alisema kama CCM haiwezi kuleta mageuzi basi mageuzi hayo yataletwa na upinzani. Lakini CCM haijashindwa kuleta mageuzi na ndiyo maana imeanza kuwatema mafisadi na kujisahihisha pale ambako imekuwa na mapungufu. Jambo hili linajionyesha hata kwa uteuzi wa mgombea wake wa urais ambaye ametoka katika majina ya watu ambao hawakutarajiwa. Mageuzi kama haya yanayofanywa na CCM wakati huu ndiyo sababu kuu iliyomfanya Kingunge Ngomale Mwiru kung’oka kwenye chama kwani alitarajia jina alilolizoea kuteuliwa lakini halikuteuliwa. Ingawa Ngombale pia kaongelea maswala ya kukiuka na kutoheshimu katiba amesahau pia kuwa CCM ilikuwa na wagombea 38 na baada ya mchujo mmoja ndiye akatokea kidedea. Haiwezekani kuwa wote 38 wangeteuliwa. Mbona huko anakokusifiwa ni mgombea mmoja tu aliteuliwa na hakuna mwingine aliruhusiwa kugombea! Je kikatiba ni nani ambaye hakufuata au kuheshimu. Pamoja na haya yote mwaka 1995 Mwalimu alivyomuondoa Lowassa kwenye orodha mbona hakusema katiba ilipingwa?

    ReplyDelete

bila kutumia lugha ya matusi na kumharibia mtu siku
yake