Mabaki ya gari aina ya Toyota Spacia yenye namba za usajili Z 511 FG, iliyokuwa ikiendeshwa na mtu anayedaiwa kuwa ni askari wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania, JWTZ, likiwa eneoa la ajali majira ya saa 8;10 mchana wa leo Oktoba 1, 2015. Kwa mujibu wa mashuhuda ajali hiyo mbaya ilitokea eneo la kijiji cha Kibele, wilaya ya Kati mkoa wa Kusini Unguja, kisiwani Zanzibar.
Mashuhuda hao walisema, gari hilo liliacha barabara na kugonga mnazi ambao uliangukia gari na baadae gari kuwaka moto. Dereva alitolewa ndani ya gari akiwa amebanwa na air bags zilizofyatuka na kuokoa uhai wake. Alipata majeraha madogo ya kuchubuka kwenye mikono yake iliyokuwa inavuja damu na kukimbizwa hospitali kwa matibabu zaidi. Dereva alikuwa peke yake ndani ya gari hilo. (Picha na Hassam Hassan)
No comments:
Post a Comment
bila kutumia lugha ya matusi na kumharibia mtu siku
yake