ANGALIA LIVE NEWS

Thursday, November 19, 2015

BODI YA MIKOPO YA ELIMU YA JUU YATOA MAJINA YA AWAMU YA NNE NA YA MWISHO YA WANAFUNZI WALIOPANGIWA MIKOPO

Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu inapenda kuwafahamisha waombaji wa mikopo kwa mwaka wa masomo 2015/2016 kuwa imetoa orodha ya AWAMU YA NNE NA YA MWISHO yenye jumla ya waombaji wa mwaka wa kwanza 718 waliopangiwa mikopo.

Majina yote ya waombaji waliofanikiwa kupangiwa mikopo kutoka katika awamu zote nne yanapatikana kupitia mtandao wa Bodi wa olas.heslb.go.tz na tovuti ya Bodi (www.heslb.go.tz). Aidha, orodha hizo pia zimetumwa vyuoni kwa ajili ya taratibu za usajili.

No comments: