Picha ya Godrey Mbiu Mngodo enzi ya uhai wake ikiwa ukumbini kwenye chakula baada ya ibada ya kumbukumbu iliyofanyika siku ya Jumamosi Octoba 31, 2015 Columbus, Ohio nchini Marekan.
Mshereheshaji mchungaji David Mngodo kwenye ukumbi wa chakula baada ya ibada ya kumbukumbu ya marehemu Godfrey Mbiu Mngodo akieleze jinsi alivyomfahamu marehemu.
Michael Mngodo akielezea jinsi baba yake alivyokua mtu wa watu na jinsi gani alivyokienzi Kishwahili. Kulia ni mtoto wake Alvin.
Margereth Mbwana mmoja ya wanafamilia akielezea jinsi alivyomfahamu marehemu Godfrey Mngodo.
Kwa picha zaidi bofya soma zaidi
Victoria Mngodo akielezea jinsi alivyomfahamu marehemu mpendwa baba yake huku akikumbuka siku alipowapeleka watoto wake kwa babu yao Dar es Salaam na kutembelea kituo cha Channel Ten ambacho zamani kilikua kijijulikana kama DTV na kuona jinsi babu yao alivyokua akifanyakazi ya utangazaji kituoni hapo.
Vincent Mngodo akimuelezea marehemu.
Kwetukia Mngodo akimuelezea baba yake yeye ndio mtoto wa mwisho wa marehemu.
Maria Mayaka Mrs Kiyashi) ambaye ni mjukuu wa marehemu akielezea jinsi alivyokua akiitwa mchumba na mareheu wakati alivyokua mdogo kama kumbukumbu yake ya babu yake Godfrey Mngodo.
Michael Mngodo akimtambulisha jirani yake Rajesh enzi hizo za Upanga.
Julie Bonzon Nyang'oro akielezea jinsi alivyofundishwa kazi ya utangazaji Channel Ten na marehemu Godfrey Mngodo.
Sunday Shomari mmoja ya wafanyakazi wa VOA akitambulisha sauti ya inayotumika kwenye idhaa hiyo kama kumbukumbu ya Godfrey Mngodo kwani yeye ndiye aliyakua mtangazaji wa kwanza wa idhaa ya Kiswahili wa VOA siku ilipoaanzishwa miaka uya mwanzo ya 1962.
Mkuu wa idhaa ya Kiswahili ya VOA Dr. Hamza Mwamoyo akimwelezea marehemu.
Wajukuu wa marehemuAgma na Kelvin wakiimba moja ya wimbo wa injili kwa ajili ya babu yao.
Teddy Mngodo akihitimisha kwa neno la shukurani kwa wale wote walioshiriki kwa njia moja au nyingine na hatimaye kufanikisha siku hiyo muhimu ya kumbukumbu ya maisha ya marehemu Godfrey Mngodo. Kulia ni mume wake Michael Mngodo.
Pr. Mwakabonga akiombea chakula.
No comments:
Post a Comment
bila kutumia lugha ya matusi na kumharibia mtu siku
yake