Wednesday, November 25, 2015

JULIUS MTATIRO "AMJIA JUU" DC WA KINONDONI KWA KITENDO ALICHOWAFANYIA MAAFISA ARDHI


PONGEZI HIZI KWA MAKONDA HAZIKUBALIKI!
Ndugu zangu, muda huu nimeona kwenye mitandao kadhaa watu wakifurahia hatua ya Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni ndugu yetu Paul Makonda kutoa amri (ambayo imetekelezwa) ya kuwaweka ndani wataalam wa ardhi ambao walishindwa kufika eneo la kazi kwa wakati.
Binafsi siungi mkono kitendo cha watendaji kuchelewa maeneo ya kazi lakini zaidi ya yote siungi mkono kitendo cha mkuu wa wilaya kuwaweka ndani watendaji kwa kosa la kuchelewa kazini.
Madhara ya kuwachekea wakuu wa wilaya pale wanapotoa amri zinazokiuka haki za msingi za wafanyakazi ni makubwa mno. Huko nyuma tulizoea mambo haya kufanywa na wakuu wa wilaya enzi za Nyerere, hatutarajii hadi leo wakuu hawa kuendesha wilaya zao kwa amri.
Ni muhimu sana masuala ya kazi yaendeshwe kwa sheria na kanuni za kazi na huyo mtu anayefurahia mamlaka ya ma DC kuweka watu ndani atakuwa na matatizo makubwa. Watu wanapaswa kuwekwa ndani kama wamefanya makosa kwa mujibu wa sheria na si kama apendavyo DC.
Tuijenge nchi yetu kimfumo zaidi kuliko ki-amri, nchi zinazoendeshwa kwa amri amri huwa hazifiki kokote, kama tutashindwa kujijenga kimfumo katika miaka hii mitano tukategemea kuendesha nchi kwa amri, matamko na mikwara - ikifika 2020 tutaulizana nini kilifanyika na sote tutabaki kusimulia matamko lukuki yaliyotolewa.
Nimalizie tena kwa kuwakumbusha kuwa "Afrika itajengwa na mifumo imara, watu imara hawawezi kuijenga Afrika maana siku moja watakufa, na kama watakufa bila kuacha mifumo imara - yale yote waliyoyafanya yatapotea haraka ".
Ndugu yetu DC, Paul Makonda, tujengeeni mfumo imara utakaofanya wafanyakazi wote kuwa kazini kwa wakati,

3 comments:

  1. DC Makonda Obeja mami kazi safiiiiii

    ReplyDelete
  2. Kwa maoni yangu huyu DC na yeye angeenda ndani sababu huwezi kuwa unawasubiri watu kwa masaa 3 hajui kuwa analipwa na walipa kodi hivyo na yeye ana kosa la kupoteza masaa 3 bila kufanyakazi akiwa analipwa na serikali kwa hayo masaa.Msubiri mtu dakika 15 kama wanachelewa endelea na kazi ama endelea na majukumu mengine. Pili ningependa kumkumbusha mtoa mada Enzi za nyerere maDC walikuwa na maamuzi ya nidhamu siyo ya kutafuta sifa kwa sababu binafsi na kutafuta vyeo kinguvu.nakumbusha rais alienda wizara ya fedha akakuta watu wengi hawapo ofisini hakuamuru wafukuzwe kazi mara moja ama kufungwa jela ingawa ana mamlaka ya kufanya hivyo, huyu DC ana upeo mdogo kiuongozi.Magufuli hataki sifa za kulazimishwa kama hizo zitamponza.

    ReplyDelete
  3. Time is money: mfanya kazi yeyote aisye fika kazini ON TIME anaachishwa kazi. tujifunze ile tabia ya kufika kazin on time kama watu wa nchi zote zilizoendelea. Mkuu wa Kinondoni ameonyesha mfano wa uongozi mzuri. Dr. Magufli angewaachisha kazi hapo hapo. HAPA NI KAZI TU

    ReplyDelete

bila kutumia lugha ya matusi na kumharibia mtu siku
yake