ANGALIA LIVE NEWS

Wednesday, November 18, 2015

Magufuli kiboko… awahenyesha Makatibu Wakuu wa Wizara


Rais Dk. John Pombe Magufuli alipofanya Mkutano na Makatibu Wakuu wa Wizara mbalimbali.

Na Waandishi Wetu

ZIARA mbili tu alizofanya Rais Dk. John Pombe Magufuli ‘JPM’ kwenye Wizara ya Fedha na kukuta wafanyakazi sita wamekwenda ‘brekfasti’ na ile ya Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) na kukuta mashine za MRI na CT Scan ziko hoi, tayari nchi imetikisika ambapo sasa kila mtumishi wa serikali analinda kibarua chake kwa kufuata masharti ya ajira.
Elisante Ole Gabriel.

Kufuatia ‘shtukiza’ hizo, sasa kila mkuu wa kitengo kwenye ofisi za serikali, anasimamia vyema uadilifu na wafanyakazi wake kwa kuwa ‘hawajui siku wala saa’ ambayo Magufuli ataibukia hapo.

Donald Mmbando

Novemba 10 na 11, mwaka huu, timu ya waandishi wa gazeti hili ilidamkia kwenye wizara mbalimbali zilizopo jijini Dar kwa lengo la kujionea wafanyakazi wanavyowahi au kuchelewa katika kipindi hiki cha ‘Hapa Kazi Tu’.

Pia, Uwazi ilitaka kujua kama makatibu wakuu wa wizara hizo ambao kwa sasa ndiyo wasimamizi wakuu baada ya kutokuwepo kwa mawaziri, wanawahi maofisini au bado wanakwenda kwa ‘mwendo wa kizamani’.

Adelhelm Meru

Saa moja na nusu juu ya alama, Uwazi lilitia timu kwenye Wizara ya Ujenzi kwenye makao yake makuu maeneo ya Posta na kukuta katibu mkuu wake, Mhandisi Mussa Iyombe ameshafika ‘siku nyingi’. Gari la katibu huyo lilikuwa kwenye maegesho.

Jengo la Wizara ya Afya

Mwandishi wetu aliweza kupiga picha, lakini kabla hajatoka, alitiwa mbaroni na walinzi wa wizara hiyo baada ya simu kupigwa getini na kujulishwa kuwa, kamera za ulinzi (CCTV) zimemwona mtu akipiga picha.

Hata hivyo, baadaye walinzi hao walimwachia mwandishi huyo kwa vile hakuwa na silaha yoyote.

Jengo la Wizara ya Nishati na Madini

Mwandishi mwingine, muda huohuo alivamia Wizara ya Habari, Utamaduni Vijana na Michezo iliyopo Posta ambapo katibu mkuu wake ni Profesa Elisante Ole Gabriel na kuambiwa na walinzi kuwa, bosi huyo alikwishakaa kwenye kiti chake.
Jengo la Wizara ya Maliasiri na UtaliiJengo la Wizara ya Uchukuzi

Ili kuendelea kujiridhisha na uchunguzi wake, Uwazi liliibukia Wizara ya Uchukuzi maeneo ya Posta na kumkuta Katibu Mkuu, Shaaban Mwinjaka ameshapita langoni kuingia ofisini kwake.

Siku ya pili, Uwazi likajihimu kwenda Wizara ya Maliasili na Utalii maeneo ya Keko na kuambiwa na mlinzi kuwa, Katibu Mkuu, Dk. Adelhelm Meru hajafika. Uwazi lilipiga kambi lakini katika hali ya kushtukiza, ndani ya dakika kumi aliingia na kuwahi muda wa kuingia kazini kwa watumishi wa serikali ambao ni saa 1:30 mpaka saa 2:00 asubuhi.

Uwazi lilibahatika kuzungumza na katibu mkuu huyo ofisini kwake kwa kumuuliza kuhusu maendeleo ya Hoteli ya Embassy iliyopo maeneo ya Posta ambayo mmliki wake ni wizara hiyo. Katibu mkuu huyo alikuja mbogo akimwambia mwandishi hawezi kujibu swali hilo kwani yeye anajua kila kitu.

Pia, Mwandishi mwingine wa Uwazi aliwasili kwenye Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii lakini katibu mkuu wake, Donald Mmbando alishafika na mlinzi aliweka ngumu kumwona kwa madai kwamba tayari alikuwa kwenye kikao cha kila siku na wafanyakazi wa wizara hiyo.

“Unajua siku hizi huwezi kukuta katibu mkuu amechelewa. Magufuli anawahenyesha ile mbaya. Sasa kama mtu hataki kazi, achelewe aone,” alisema mfanyakazi mmoja wa wizara hiyo bila kutaja jina lake.

4 comments:

Anonymous said...

Safi sana baba magufuli umeanza vizuri,tena wawekewe kabisa mashine ya kupunch in and out ,tukiendelea na mwendo huu nchi itafika mbali sana,hapa kazi tu,ndio maana nchi za wengine zinaendelea sababu wanaheshimu kazi zao,ubarikiwe baba na tunakuombea usije ambukizwa gonjwa baya la rushwa na wana ccm wenzako

Anonymous said...

KUNA NINI KIPYA?KIBOKO KACHAPA NANI MAGUFULI?KAFUKUZA KAZI NANI? KULE KUITA WATENDAJI UNAMWAGA "SIFA" "KIBOKO ".YALE YALE.WALE WALE.UTENDAJI KAZI SERIKALINI SASA HIVI UMESHUKA,UMESHUKA,UMESHUKA.NI 30% HATUJAONA MABADIRIKO,HAKUNA MABADIRIKO, CCM SI YA MABADIRIKO.MATOKEO BEI ZA BIDHAA ZINAZIDI KUPANDA.LEO TUNAPOONGEA JIULIZE ORODHA YA MABADIRIKO MAKUBWA SANA MHE.LOWASSA ANGESHAYATEKELEZA.TUNASIKITIKA, TUNALIA.

Anonymous said...

Utasikitika na kulia sana kwa sababu ya utahira ulionao! Fisadi wako amekuwa mtumishi wa umma kwa miaka karibu arobaini na hana track record ya kujivunia; wananchi watamkumbuka kwa ufisadi papa tu!

Anonymous said...

Hahahaaaa uwiii eti kwa utahira wako