ANGALIA LIVE NEWS

Wednesday, November 18, 2015

Mbunge Dkt Harrison Mwakyembe "afikishwa mahakamani"


ALIYEKUWA mgombea wa Ubunge kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) jimbo la Kyela Mbeya,Abraham Mwanyamaki amefungua kesi ya kupinga matokeo yaliyompa ushindi Dr,Harrison Mwakyembe (CCM) katika mahakama kuu kanda ya Mbeya akidai yalikuwa na kasoro Lukuki.
Akizungumza jana na waandishi wa habari kwenye mahakama hiyo,Mwanyamaki alisema Dr, Mwakyembe hakushinda kihalali katika uchaguzi huo ambapo alipoona ameshindwa aliliamuru jeshi la polisi kuwatawanya watu kwa kuwapiga mabomu kisha kujitangazia ushindi kinyume na taratibu.

Alisema katika mchakato mzima kuanzia kura za maoni Mwakyembe alitoa Rushwa ya pesa na vitu kadhaa kwa wananchi akiwarubuni kumpa kura wakati wa uchaguzi ikiwemo kutoa kauli chafu katika kampeni na kuwa wakati wa majumuisho ya kuhesabu kura alimuamuru mkuu wa polisi kumpiga msimamizi wake.

Kwa upande wa mkurugenzi wa uchaguzi ambaye pia ni mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya hiyo,Clement Kasongo,alisema alikuwa na kila dalili za kuchakachua matokeo hayo baada ya kuingiza vituo hewa ambavyo havikuwepo kwenye orodha pomoja na mambo mengine.

Mwanasheria aliyeishika kesi hiyo,Benjamin Mwakagamba kutoka kampuni ya Advocates, Notaries Public Commissioners for oaths ya jijini Dar es Salaam, alisema kutokana na kuipitia nakuangalia kasoro hizo ameona kuna umuhimu wa kufungua kesi akiwa na matumaini ya kushinda kutokana na mazingira yenyewe.

Alisema mteja wake amefungua kesi ya kihistoria namba 2 ya mwaka 2015 akiwashitaki watu watatu ambao ni mkurugenzi wa tume ya Uchaguzi Clement Kasongo, namba 2 ni Harrison Mwakyembe na watatu ni mwanasheria wa halmashauri kwa kukiuka taratibu za uchaguzi wakishirikiana kuchakachua matokeo.

Alisema endapo haki itatendeka anauhakika wa kushinda kesi hiyo na endapo haki haitatendeka watakata rufaa kwenye mahakama za juu kwa kuwa ushahidi wanao jinsi Dr,Mwakyembe alivyopora ushindi huo akidaiwa kutumia cheo chake cha uwaziri kulitumikisha jeshi la polisi kuvunja kanuni za uchaguzi.

Wananchi kwa upande wao wakiongozwa na Merry Mwakipesile walisema wamesafiri kutoka wilayani kyela hadi mkoani Mbeya kuhakikisha kesi hiyo inafunguliwa ambapo alisema wao kama wananchi wanao ushahidi wa kutosha jinsi Mwakyembe na Tume walivyojipa ushindi huku wananchi wakipigwa na kuteswa.

Alisema kutokana na mazingira ya jimbo la Kyela wananchi walivyokuwa wakimzomea kila kona Dr,Mwakyembe baada ya kuwa mmoja kati ya wabunge mizigo nchini alivyolitelekeza jimbo hilo likiwa hoi,alijipanga kwa gharama kubwa ya kifedha kuhakikisha anashinda kwa nguvu.

Alisema licha ya kutumia kila njia ya kuhakikisha anashinda,lakini wao walimchagua mgombea wa chadema Abraham Mwanyamaki kwa kumpa kura za mtikisiko na kuwa cha ajabu wakashangaa wanapigwa mabomu bila sababu huku Mwakyembe akijitangaza mwenyewe kuwa ameshinda.

Debora Mwakipesile mkazi wa Kyela,alisema yeye ni mmoja wa wahanga walioteswa na kudharirishwa na jeshi la polisi na kuvunjwa mkono baada ya kukamatwa na kutiwa nguvuni huku baadhi ya askali wakimdharirisha kwa shinikizo la Mwakyembe.

Alisema kutokana na hali hiyo wao kama wananchi hawapo tayari kufanya kazi na Mwakyembe kwa kuwa sio chaguo lao ni chaguo la serikali na kuwa mbunge wao wanayemhitaji ni Abraham Mwanyamaki.
Paparazi blog

5 comments:

Anonymous said...

Kazi ipo kwa sababu Dk mwakyembe ni mwanasheria sasa ingawa wanasema mganga hajigangi lakini siku zote huwa anawafahamu wanganga wazuri zaidi mtaani kuliko mtu wa kawaida sasa tusubiri na tuone. Cha msingi zaidi ni hofu kuu iliowajaa akina Lowasa na mafisadi wote Tanzania yakwamba Dk mwakyembe yupo kwenye rada za Dk magufuli ya kumkabizi uwaziri mkuu na kitu hicho kikitokea usishangae ukasikia lowasa kahamishia makaazi yake nje ya Tanzania. Huyo aliefungua kesi yeye kibaraka tu kuna watu nyuma yake wanamtumia. Lakini sidhani kama itafanya kazi.

Anonymous said...

Ni sawa sawa mwakyembe kufikisshwa mahakamani.ule ulikua ni wizi mkubwa wa kura.mimi ni wa jimbo hilo la kyela.itakuaje kwenye kuhesabu kura mara mbili zote mgombea wa wananchi alikuwa anaongoza kwa zaidi ya kura7000 ghafla tukaarifiwa vipo vituo vinne walikua hawajaleta matokeo,tulipouliza ni vipi kwa majina msimamizi akionyesha wazi upendeleo na majigambo akawa anajibu si kazi yetu kuvifahamu. SASA MAHAKAMA ITABIDI IVIFAHAMU.WIZI UNA MWISHO MBAYA.

Anonymous said...

Hiyo ni hofu kubwa iliyowatanda mafisadi, kwa kuhofia kuwa Mwakyembe atakuwa Waziri Mkuu. Na Magufuli akimpa hiyo nafasi, mafisadi bai bai. Sasahavi mafisadi papa akina Lowassa wanatumia kila njia kumchafua Mwakyembe, ee MUNGU msaidie Magufuli .

Walikuwa wapi siku zote kufungua hiyo kesi? Mpaka leo wamesikia jina la Mwakyembe linatajwa kila kona, wanaanza kujihami.

Anonymous said...

Hiyo ni hofu kubwa iliyowatanda mafisadi, kwa kuhofia kuwa Mwakyembe atakuwa Waziri Mkuu. Na Magufuli akimpa hiyo nafasi, mafisadi bai bai. Sasahavi mafisadi papa akina Lowassa wanatumia kila njia kumchafua Mwakyembe, ee MUNGU msaidie Magufuli .

Walikuwa wapi siku zote kufungua hiyo kesi? Mpaka leo wamesikia jina la Mwakyembe linatajwa kila kona, wanaanza kujihami.

Anonymous said...

Mwakyembe alishajitoa kwenye kinyanganyilo cha uMP pale alipoanza kujinzumzia yeye mwenyewe kupitia wapambe wake. Pili ili tena ni kumdhalilisha tu Hana sifa hata kuwa mbunge nadhani kama mpinzani akiwa na ushaidi wa msingi watampiga chini.