Msanii Q Chief amesema muziki wa Bongo umetawaliwa na siasa, kitendo ambacho kinawachanganya wasanii na kufanya washindwe kufanikiwa katika mambo yao ya kimuziki
Q chief ameyasema hayo kwenye Planet Bongo ya East Africa Radio, na kueleza kuwa kitendo hicho kinaharibu muziki na wasanii kwa ujumla, na kuwataka wasanii hao kutafuta mbinu mbadala ya kujikwamua katika hilo.
"Kuna politics nyingi sana nyuma ya huu muziki, siasa ambazo kwa namna moja au nyingine zinawademoralize wasanii, kwa sababu watu wana talent zao, watu wana vision zao lakini wamewekewa limitation ya vile vitu wanakusudia kuvifanya, kwa hiyo we ukiona wanaweka bariers nyingi you should find means ya ku over come hiyo situation na kuweza kufika pale ambapo unakusudia.
Pamoja na hayo Q Chief ameendelea kusema kwamba kwa sasa hategemei kufanya muziki unaokubalika nyumbani tu, na kufunikwa na wasiojua muziki kwa kuwa wanakubalika na jamii, bali analenga kutengeneza muziki utakaokubalika nje ya Tanzania.
"Mi sitegemei kuimba Manzese sijui Buguruni, i want to go kwenye competition ya watu wengi ambao wanajua muziki, kwa sababu wananijenga, lakini unacompete na watu ambao hawajui alafu yeye ndio namba moja, inauma sana", alisema Q Chief.
No comments:
Post a Comment