Mbunge wa Jimbo la Mbeya Mjini Mhe. Joseph Mbilinyi
a.k.a Sugu na Mbunge wa jimbo la Mikumi Mhe.
Joseph Haule a.k.a Professor Jay, ni wasanii wa
muziki ambao wamefanikiwa kuingia kwenye Bunge la
11 baada ya kushinda kwenye uchaguzi wa mwaka
Kupitia 255 ya XXL Sugu ambaye alikuwa Mbunge
kwenye bunge lililopita, amempa ushauri Professor
ambaye ndio ameingia mjengoni kwa mara ya kwanza
kuhusu malalamiko kutoka kwa wasanii.
“Unajua wasanii wamekuwa wakilalamika kuhusu
uwepo wangu mjengoni, ngoja niseme kitu kwa
Proffesor Jay, naomba atambue yeye ni Mbunge wa
Mikumi na hakuna jimbo la Wasanii, kama mimi nilivyo
Mbunge wa Mbeya Mjini. Tufanye kazi kwa ajili ya
maendeleo ya Wananchi wetu waliotuchagua. Kwa
sababu Wasanii wamekuwa na tabia ya kuongea kuwa
tunashindwa kuwasaidia sisi sio wabunge wa Wasanii
naomba ieleweke”. alisema Sugu.
Sugu aliendelea;
“Kuna Wasanii wengine walikuwa hawakupi hata
support kipindi cha Kampeni ila ukishinda na ukaingia
bungeni, ndio wa kwanza kukutupia lawana.”
No comments:
Post a Comment