Sunday, November 1, 2015

Obama aing'oa Burundi kutoka kwenye AGOA

'Burundi haijafanya jitihada zozote za kurejesha amani na utangamano'' Obama.

Marekani imeiondoa Burundi kutoka kwenye mikataba yake ya kibiashara AGOA iliyowezesha mataifa ya Afrika kuingiza bidhaa zao katika soko la Marekani bila kulipa kodi.

Katika barua aliyoiandikia bunge la Congress , rais Barrack Obama ameelezea kuwa amechukua hatua hiyo baada ya kushuhudia kushuka kwa viwango vya demokrasia katika taifa hilo la Afrika ya Kati.

''Burundi haijafanya jitihada zozote za kurejesha amani na utangamano'' Obama.

Obama alisema kuwa badala ya kuimarika kidemokrasia, Burundi inaendelea kushuhudia wapiganiaji wa haki za kidemokrasia wakikamatwa na kufungwa jela huku wengine wengi wakiuawa kwa kudai haki zao za kikatiba zifwatwe.

Aidha Obama ameelezea kuwa hatua ya serikali ya rais Nkurunziza ya kuwanyamazisha makundi ya wapinzani kwa kuwashika kuwaua na hata kuwatesa ni kinyume na maadili ya taifa linalodai kuzingatia demokrasia.

Marufuku hiyo ya Burundi inaanza kutekelezwa mwezi januari mwakani.

Burundi ilitumbukia katika mzozo wa kisiasa na kukumbwa na machafuko punde baada ya rais Pierre Nkurunziza kutangaza nia ya kuwania muhula wa tatu kinyume na katiba ya taifa.

Aidha kulitokea jaribio la mapinduzi lakini likazimwa.

Nkurunziza alishiriki uchaguzi huo na akashinda, hata hivyo kumeendelea kuwa na visa vya maandamano,mauaji na kutoweka kwa wapinzani wake.

Takriban watu 200 wameuaawa tangu machafuko yaanze mwezi Aprili

Inakisiwa kuwa watu 200,000 wametoroka makwao na sasa wanaishi kwenye kambi za wakimbizi katika mataifa jirani.

Mpango wa AGOA (African Growth and Opportunity Act) ulianzishwa yapata muongo mmoja uliopita ilikuzisaidia mataifa maskini ya Afrika kuuza bidhaa zao katika soko la Marekani.

4 comments:

  1. Tanzania will be next,I can't wait

    ReplyDelete
  2. That's good Obama, watch African very close so many dictators. Screw them

    ReplyDelete
  3. SASA HAMIA TANZANIA OBAMA.CCM NA MUSTAKHABARI WA ZANZIBAR.BARA TUMEIBIWA KURA, SAWA TUMEKUBALI SASA, ZANZIBAR,HAPANA,HATUTOKUBALI.MHUSIKA MKUU WA MATATIZO YOTE HAYA KIKWETE.MHE.OBAMA KWA SASA,SITISHA MISAADA YA MAREKANI KWA TANZANIA HUSUSANI AGOA NA MILENIUM CHALLENGE ACCOUNT MPAKA SERIKALI ITAKAPOJIREKEBISHA MATUMIZI,NA UWAZI.MISAADA YOTE ILIINGIA KWENE MFUKO WA KAMPENI WA CCM,WAKAWAKANDAMIZA WAPIGA KURA KWA KUWALETEA WALE AMBAO WALISHINDWA.SIMAMISHA MISAADA YOTE.

    ReplyDelete
  4. Obama akihamishia panga lake la kuwakata wapuuzi Tanzania lowasa atakuwa wa kwanza.

    ReplyDelete

bila kutumia lugha ya matusi na kumharibia mtu siku
yake