ANGALIA LIVE NEWS

Saturday, November 21, 2015

Tenga apata mrithi wake Cecafa

RAIS wa Shirikisho la Soka la Sudan, Dokta Jaffar Mutasim amechaguliwa kuwa Mwenyekiti mpya wa Baraza la Vyama vya Soka Afrika Masharikina Kati (Cecafa) kuchukuwa nafasi ya aliyekuwa Mwenyekiti wa chama hicho, Mtanzania Leodegar Tenga baada ya kuongoza kwa miaka nane.

Mutasim aliibuka mshindi kwenye uchaguzi wa chama hicho, uliyofanyika hapo jana katika hoteli ya Intercontinental mjini Addis Ababa, Ethiopia. Mutasim alipata kura sita kati ya kumi za wanachama wa Cecafa na kumzidi Mganda, Lawrence Mulindwa aliyepata tatu huku Rais wa Shirikisho la Soka la Rwanda (Ferwafa), Vincent Nzamwita akipata moja,Rais wa Shirikisho la Soka la Ethiopia, Juneydin Bashar alijiondoa dakika za mwisho.

Akizungumza mara baada ya uchaguzi huo, Mutasim alisema “Hakuna mshindi katika uchaguzi kwani mshindi siku zote atabaki kuwa Cecafa. Nawashukuru wanachama wenzangu kwa kura walizonipa, serikali ya Ethiopia kwa sapoti yao ikiwemo kuandaa michuano ya mwaka huu na mchango wao katika chama hiki kwa ujumla. Kwa mshikamano, tunaweza kufanya kazi vizuri ili kufikia malengo yetu kama eneo hili la Cecafa,” alisema.

Mkutano wa jana Ijumaa umehudhuriwa na viongozi wote wa Cecafa,Kenya ikiwakilishwa na Makamu wa Rais wa Shirikisho la Soka la Kenya (FKF) Robert Asembo. Wagombea wa kiti cha urais cha Fifa, Jerome Champagne na Prince Ali. Mkutano huo wa kawaida hufanyika kila mwaka kabla ya kuanza kwa michuano ya Kombe la Challenji ambayo yanafunguliwa rasmi leo Jumamosi.
MWANANSPOTI

1 comment:

Anonymous said...

Kuna taarifa kwamba wajumbe wa Afrika nao pia walipokea fedha za kibindoni toka kwa Bwana Blatter. Tenga atasaidia kwa kuwa muwazi na mkweli alipata kiasi gani ama alijua nini kilikuwa kinaendelea. Asijitoe tu.